TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 30.07.2014
[BARAKAEL .N. MASAKI – ACP]
- MZEE WA MIAKA 75 AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
- MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MZEE MMOJA
MWENYE UMRI WA MIAKA 75 ALITAMBULIKA KWA JINA LA DAIMONI MATATA, MKAZI
WA KIJIJI CHA LUSINGO ALIUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI
SEHEMU ZA SHINGONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
TUKIO HILO
LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 02:00 HUKO KATIKA KIJIJI
CHA LUSINGO, KATA YA SONGWE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA
MBALIZI, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILO BADO KINACHUNGUZWA. AIDHA
MTU MMOJA AMBAYE NI MTOTO WA MAREHEMU AITWAYE WATSON DAIMONI (53) MKAZI
WA KIJIJI CHA LUSINGO AMEKAMATWA KWA MAHOJIANO KUHUSIANA NA TUKIO HILI.
MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI – MBALIZI KWA
UCHUNGUZI WA KITABIBU. UPELELEZI ZAIDI JUU YA TUKIO HILI UNAENDELEA.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL .N.
MASAKI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA
TUKIO HILI AZITO KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAO. AIDHA ANASHAURI FAMILIA ZIWE NA UTAMADUNI WA
KUKAA NA KUTATUA KERO NA CHANGAMOTO MBALIMBALI AMBAZO ZINAJITOKEZA
KATIKA KAYA ZAO ILI KUEPUKA MADHARA/MATATIZO YANAYOWEZA KUJITOKEZA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTEMBEA
KWA MIGUU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA BARAKA ZAWADI MJEMWA (31)
MFANYABIASHARA NA MKAZI WA MIKOROSHINI – KYELA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA
GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.604 BCS AINA YA TOYOTA NOAH LIKIENDESHWA
NA DEREVA AITWAYE ASAJILE AYUB (35) MKAZI WA KASUMULU KULIGONGA GARI
JINGINE LENYE NAMBA ZA USAJILI T.649 ALB AINA YA TOYOTA HILUX LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE MUSA MWALUBANGE (32) MKAZI WA KIJIJI CHA
MBUGANI NA KISHA KUPOTEZA MWELEKEO NA KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU HUYO.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 29.07.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO
KATIKA KIJIJI CHA ILAMBO, KATA YA ITOPE, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA
KYELA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI BAADA YA GARI T.604 BCS KUTAKA
KUYAPITA MAGARI YALIOKUWA MBELE YAKE BILA KUCHUKUA TAHADHARI. DEREVA
AMEKAMATWA.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL .N.
MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA
AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Imetolewa na kusainiwa na:
[BARAKAEL .N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment