Thursday 31 July 2014

chicha_0d0a3.jpg Mabingwa wa Spain, Atletico Madrid wanataka kuwasajili Santi Cazorla, 29, kutoka Arsenal, Fernando Torres, 30, kutoka Chelsea na Chicharito, 26 kutoka Manchester United (Daily Star), Chicharito amekiri kuwa hana uhakika kama ataendelea kuwepo Old Trafford akisema "Mungu pekee ndio anajua" kuhusu hatma yake (Guardian), Tottenham wanatarajia kurejea na fedha zaidi kumtaka kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin, licha ya Saints kusema mchezaji huyo hatoruhusiwa kuondoka (Daily Telegraph), Sporting Lisbon wamewaambia Southampton kuwa watalazimika kutoa pauni milioni 16 kumsajili beki kutoka Argentina Eric Dier, 20 (Daily Telepgraph), Marouanne Fellaini, 26 amekubali kujiunga na Napoli ya Italia, lakini Manchester United wanataka pauni milioni 18 kwa mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa pauni milioni 27.5 mwaka jana (Daily Star), meneja wa Sunderland Gus Poyet amethibitisha kuwa wameanza tena mazungumzo ya kumsajili Fabio Borini, 23, kutoka Liverpool (Daily Express), Arsenal wanaweza kufufua mazungumzo ya kumsajili Sami Khedira, 27, kwa kuwa Real Madrid wanataka kumuuza kiungo huyo (Daily Mirror), Juventus wamekubali dau la pauni milioni 47 kutoka Manchester United kumsajili Arturo Vidal, 27, na mchezaji huyo wa Chile amekubali maslahi binafsi na Old Trafford (CaughtOffside), matumaini ya Newcastle ya kumsajili mshambuliaji Alexandre Lacazette, 23, kwa pauni milioni 10 yamegonga mwamba baada ya mchezaji huyo wa Ufaransa kusaini mkataba mpya na klabu yake (Newcastle Cronicle), Napoli wamewapa Manchester United Dries Mertens kubadilishana na Marouanne Fellaini (Daily Express), Karim Benzema amekubali kusaini mkataba mpya na Real Madrid hadi mwaka 2018 wenye thamani ya euro milioni 7 kwa mwaka (El Confidencial), Bayern Munich wameanza kumfuatilia winga wa Real Madrid Angel Di Maria ambaye anasakwa pia na Manchester United na Paris Saint-Germain (AS). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Share na wapenda soka wote. Cheers!!(E.L)

0 comments:

Post a Comment