BONDI toka
nchini Malawi Jonson Adam amewasili mjini songea mkoani Ruvuma tayari kwa pambano la roundi 10 litakaofanyika tarehe 29
siku ya iddi dhidi ya bondia toka mkoani humo musa omari maarufu kwa jina la
chitepete ambapo maandalizi ya mtanange huo yanaendelea vizuri na mgeni Rasimi atakuwa Francis cheka toka Morogoro.
Kulia ni bondia musa omari toka songea |
“katika rekodi yangu sijawai pigwa ila nimetoa sare
mara mbili hivyo wanaruvuma na watanzania kwa ujumla wasitegemee mteremko
nimekuja kufanya kazi na sio kucheza.
Vile vile
mwalimu ambaye amekujanae mkoani Ruvuma Toka kyela mkoani mbeya ambao bondia
huyo alifikia muddy Eliya alisema Jonson adam amekuja kufundisha ngumi hapa
nchini ambapo musa kama ajajiandaa ajiandae kwani anaweza kufia uwanjani siku
hiyo kwa kuwa Adam ni bondia mzuri.
Lakini kwa
upande wake bondia toka Songea Musa omari
amewatoa hofu wanaruvuma na Tanzania kwa ujumla kwa kusema kuwa
atahakikisha anamaliza pambano Roundi ya tatu kutokana na maandalizi ambayo
amefanya na watu wa Malawi wajiandae kupokea msiba siku ya Iddi.
licha ya kuwepo kwa mpambano huo lakini Mitanange mingine
Itakayopigwa siku hiyo ni pamoja na jams Ntanga wa songea atakipiga na Furaha
ndengenye toka Kyela pia Alibobu wa njombe ataonyeshana kazi na bondia toka
songea,pia kutakuwepo na wasanii mbali mbali kama zimwi,linko pamoja na domo la
mamba toka jijini Dar .
musa omari |
0 comments:
Post a Comment