Taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa mbeya kwa vyombo vya habari “press release” tarehe 31.07.2014.
Watu wanne wafariki dunia na wengine 51 kujeruhiwa katika ajali ya gari matundasi wilayani chunya.
Mtu mmoja afariki dunia katika ajali ya barabarani jijini mbeya.
Mtoto wa miaka mitatu afariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi cha mchanga wilayani chunya.
Mtoto wa miaka kumi afariki dunia baada ya kupigwa na shoti ya umeme.
Katika tukio la kwanza:
Watu
wanne waliotambulika kwa majina ya 1. paulo mwasanga (18) mkazi wa
kitongoji cha matundasi ‘b’ 2. wedi angolwise (21) mkazi wa matundasi 3.
salome mwakibete (13) mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi
sambilimwaya na 4. obedi mwakamela (25) mkazi wa matundasi wamefariki
dunia papo hapo baada ya gari lenye namba za usajili t.595 chu aina ya
fuso tipper likiendeshwa na dereva asiyefahamika jina kipinduka katika
kijiji cha matundasi wilayani chunya.
Ajali
hiyo ilitokea mnamo tarehe 30.07.2014 majira ya saa 16:00 jioni huko
katika kitongoji cha matundasi “b”, kijiji cha matundasi, kata ya
matundasi, tarafa ya kiwanja, wilaya ya chunya, mkoa wa mbeya katika
barabara ya chunya/makongolosi.
gari
hilo lilikuwa likitokea kijiji cha sambilimwaya kuelekea kijiji cha
matundasi likiwa limebeba wachezaji wa mpira wa miguu na mashabiki.
aidha katika ajali hiyo watu 51 walijeruhiwa, kati yao 26 walitibiwa na
kuruhusiwa na wengine 25 wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya chunya
wakiendelea kupatiwa matibabu. chanzo cha ajali ni mwendo kasi, dereva
alikimbia mara baada ya tukio na juhudi za kumtafuta zinaendelea.
kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi barakael
.n. masaki anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya
moto hasa kwa kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili
kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. aidha anatoa wito kwa yeyote mwenye
taarifa za mahali alipo mtuhumiwa azitoe katika mamlaka husika ili
akamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
katika tukio la pili:
mtu
mmoja aliyetambulika kwa jina la wile peter ambaye alikuwa abiria
katika pikipikiamefariki dunia baada ya gari lenye namba za usajili dfp
0036 aina ya benz mali ya shirika la umeme tanesco lililokuwa
likiendeshwa na patrick mhagama (46) mkazi wa ilomba jiji mbeya kumgonga
mpanda pikipiki asiyefahamika jina wala makazi yake na kusababisha kifo
kwa abiria huyo.
Ajali
hiyo imetokea mnamo tarehe 31.07.2014 majira ya saa 16:45 jioni huko
nzovwe, kata ya nzovwe, tarafa ya iyunga, jiji na mkoa wa mbeya. chanzo
cha ajali kinachunguzwa. dereva amekamatwa na gari lipo kituoni. mwili
wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa mbeya.
Kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi barakael .n.
masaki anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto
hasa kwa kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka
ajali zinazoweza kuepukika.
Katika tukio la tatu:
Mtoto
mwenye umri wa miaka mitatu aliyetambulika kwa jina la pascalia jifula
ngasa amefariki dunia baada ya kuangukiwa na kufunikwa na kifusi cha
mchanga katika kitongoji cha chizya wilayani chunya.
Tukio
hilo limetokea mnamo tarehe 30.07.2014 majira ya saa 08:300 asubuhi
huko katika kitongoji cha chizya, kijiji cha mwambani chini, kata ya
mwambani, tarafa ya kwimba, wilaya ya chunya, mkoa wa mbeya. wakati
tukio hilo linatokea, mtoto huyo alikuwa akicheza na watoto wenzake
kwenye gema la mchanga na ndipo kifusi kumuangukia na kumfunika.
Kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi barakael
.n. masaki anatoa wito kwa wazazi na walezi kuwa makini na watoto wadogo
kwa kuangalia mazingira ya maeneo yao ili kuepuka madhara yanayoweza
kujitokeza.
katika tukio la nne:
Mtoto
wa miaka kumi aliyefahamika kwa jina la jerry jested, mwanafunzi na
mkazi wa mlowo wilayani mbozi alikutwa amekufa chumbani kwake baada ya
kupigwa na shoti ya umeme.
Tukio
hilo limetokea mnamo tarehe 30.07.2014 majira ya saa 06:00 asubuhi huko
katika kata ya mlowo, tarafa ya vwawa, wilaya ya mbozi, mkoa wa mbeya.
inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni baada ya marehemu kulamba nyaya
za umeme ambazo zilikuwa karibu na kitanda chake hali iliyopelekea
kupigwa shoti na kusababisha kifo chake.
Kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi barakael
.n. masaki anatoa wito kwa wazazi na walezi kuwa makini na watoto wadogo
kwa kuangalia mazingira ya maeneo yao ili kuepuka madhara yanayoweza
kujitokeza ikiwa ni pamoja na kuweka mbali vitu vya hatari kwa watoto.
imetolewa na kusainiwa na:
[barakael .n. masaki – acp]
kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mbeya.