Mshauri
wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kushoto), akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam wakati wa
majumuisho ya ziara ya Profesa Pais mara baada ya kutembelea mikoa
kadhaa nchini kuangalia ukubwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti
(katikati), Daktari Bingwa wa Ugonjwa Saratani ya Matiti kutoka India,
Profesa Anthony Pais , na kulia Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer
Wines and Spirits LTD, Benedicta Rugemalira.
Mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits LTD, Respicius Didace.akichangia mada. Mkurungenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog, John Bukuku (kushoto), akitoa maoni yake wakati wa mkutano.
Mliki wa Mtandao wa Kamanda wa Matukio blog, Richardi Mwaikenda akichangia mada wakati wa mkutano huo.
Mshauri
wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kulia), daktari bingwa
wa ugonjwa saratani ya matiti kutoka India, Profesa Anthony Pais
(wakwanza kushoto), Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and
Spirits LTD, Benedicta Rugemalira wakiwa kwenye picha ya pamoja mara
baada kumalizika kwa mkutano huo.
Mshauri
wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kushoto) na Mkurugenzi
wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits LTD, Benedicta Rugemalira
(kulia), wakimpa zawadi Profesa Pais baada ya kutoa majumuisho.
……………………………………………………….
HATUA mahususi na za haraka zinahitajika kukabiliana na ugonjwa wa saratani ambao umegeuka kuwa tishio hapa nchini.
Hayo yalisemwa na daktari bingwa
wa ugonjwa huo, hususani saratani ya matiti kutoka India, Profesa
Anthony Pais, jana jijini Dar es Salaam katika majumuisho ya ziara yake
aliyoifanya katika mikoa mbalimbali kuangalia ukubwa wa ugonjwa huo.
Akiwa ameongozana na viongozi wa kampuni ya Mabibo Beer Wines and
Spirits Limited, iliyodhamini ziara hiyo, daktari huyo ameshauri kuwa
kuna umuhimu wa kujenga kituo kikubwa cha kimataifa hapa nchini
kitakachoshughulikia ugonjwa huo ili kupunguza gharama za kupeleka
wagonjwa nje ya nchi.
“Nimegundua kuna vituo viliwili,
kimoja Ocean Road na Hospitali ya Muhimbili. Lakini tatizo la saratani
kwa sasa Tanzania ni kubwa na linahitaji kushughulikiwa kwa haraka.
Ningependelea kuwepo na vituo viwili vikubwa. Kimoja Mwanza na kingine Bukoba ili kuhudumia hata nchi jirani,” alisema.
Ameeleza kuwa katika ziara
aliyoifanya katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Kagera na Mwanza,
amegundua kuwa kuna aina kuu tatu za saratani ambazo zinasumbua wananchi
wengi na kumekuwepo na msululu wa wagonjwa wakipelekwa India kupata
matibabu kwa gharama kubwa.
Dk Pais amezitaja aina hizo za
saratani kama saratani ya matiti, saratani ya kibofu cha mkojo na
saratani ya shingo ya uzazi. Alieleza kuwa wagonjwa wengi wamekuwa
wakigundulika kuwa na saratani hizi wakati tayari zimeshafikia hatua ya
kutisha.
“Hivyo tukiwa na vituo hapa hapa
Tanzania vya kupima na kutibu ugonjwa huu itasaidia wagonjwa kujulikana
mapema na baadae kupata tiba haraka tena kwa bei nafuu. Mimi niko tayari
kutoa mafunzo kwa wahusika mbalimbali kutoka madaktari hadi wahudumu.
Kwa pamoja tunaweza,” alisema.
Naye Mshauri wa kujitegemea wa
kimataifa wa Mabibo, James Rugemalira, ambaye kampuni yake husambaza
vinywaji aina ya Windhoek Larger na Windhoek Draught hapa nchini,
amemshukuru daktari huyo kwa kukubali kuja na kwa ushauri wake ambao
utasaidia sana katika kukabiliana na ugonjwa huo.
Ameeleza kuwa mara kampuni yake
itakapopokea taarifa ya kitaalaam kutoka kwa daktari huyo, Mabibio
itaaanzia mchakato utakaofanikisha ujenzi wa vituo vingine vya
kushughulikia ugomjwa wa saratani ili kupambana na tatizo hili hapa
nchini.
0 comments:
Post a Comment