SEMINA
ya Kamata Fursa Jitathimini,Jiamini,Jiongeze inayoendeshwa sambamba na
burudani za Fiesta 2014, jana imeendelea kwa kuwapatia dira ya maisha na
namna ya kuwafanya wajikwamue kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi
wakazi wa Mkoa wa Tabora mjini ndani ya ukumbi wa chuo cha TEKU,kilichopo katikati ya mji wa Tabora.
Semina
hiyo ambayo imeongozwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds
Media Group, Ruge Mutahaba (pichani juu) ilikuwa ya aina yake, kwani
baadhi ya vitu na mbinu alizowapatia wakazi wa Mkoa wa Tabora,wengi wao
wameonesha kuvutiwa nayo kutokana na mafunzo,maelekezo na mbinu
mbalimbali za kupambana na changamoto zinazowakabili/zitakazowakabili
katika miradi yao mbalimbali wanayotarajia kuianzisha ama
wamekwishaianzisha.
Msanii muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Weusi,Niki wa Pili akizungumza na vijana
mbalimbali waliokuwa wamegawanywa katika makundi ili kusikiliza mipango na miradi waliyonayo na namna wanavyoiendeleza,lakini pia Washiriki hao walielezwa namna ya kujikwamua na changamoto wanazokumbana nazo katika kuendeleza miradi yao,ikiwamo na namna ya kujitafutia soko ,jambo ambalo Washiriki hao wamekiri wazi kuwa ndio changamoto yao kubwa katika shughuli zao za ujasiliamali.
mbalimbali waliokuwa wamegawanywa katika makundi ili kusikiliza mipango na miradi waliyonayo na namna wanavyoiendeleza,lakini pia Washiriki hao walielezwa namna ya kujikwamua na changamoto wanazokumbana nazo katika kuendeleza miradi yao,ikiwamo na namna ya kujitafutia soko ,jambo ambalo Washiriki hao wamekiri wazi kuwa ndio changamoto yao kubwa katika shughuli zao za ujasiliamali.
Meneja wa Maxcom Africa, ‘Max malipo’, Bernard Munubi akiwa katikati
ya vijana akiwaeleza namna ya kufanikiwa katika shughuli zao kimaendeleo
na pia kuwapatia mbinu za kupambana na changamoto na hatimae kuelekea
kwenye kilele cha mafanikio .Bernad pia aliwaeleza washiriki hao kwa
wale ambao wanafikiria kuanza miradi ya ujasiliamali,kwamba si vibaya
wakaanza kujaribu kujitafutia maendeleo kupitia mashine na Max Malipo na
kujionea wenyewe namba zinavyoweza kusaidia kiasi kikubwa cha umaskini
miongoni mwao.Mnubi alisema kuwa mmpaka sasa mashine hizo zimewaletea
mafanikio makubwa ya kiuchumi watu wengi.
Mmoja
wa Wajasiliamali kutoka mjini Tabora ,Dada Flora Zakaria ambaye
amejiunga kwenye moja ya kikundi kinachofanya shughuli mbalimbali
kupitia kikundi chao kiitwacho JACANA Natural Products,akionesha aina ya
sabuni zilizotengenezwa na kikundi chao,ambapo pia kikundi hicho
hujishughulisha na utengenezaji wa vipodozi vya asili kwa akina mama
pamoja na mafuta ya aina mbalimbali.Flora alieleza kuwa wamekuwa
wakijitahidi kutengeneza bidhaa mbalimbali lakini changamoto yao kubwa
imekuwa ni namna ya kupata soko la kuziuza bidhaa zao.
Baadhi
ya wanafunzi wa chuo cha VETA wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa
zikichambuliwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds
Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba (hayupo pichani).Ambapo washiriki wa
semina hiyo waliunda vikundi na kubainisha wana miradi gani ama
wanatarajia kuanza kufanya miradi gani,ili kusaidia kutatua vikwazo na
kutoa miongozo kwa namna moja ama nyingine.
Niki
wa Pili akifafanua jambo kwa baadhi ya Washiriki wa Semina hiyo ya
Fursa,ambayo imekuwa ikiwavutia watu wa rika mbalimbali wakiwemo vijana
kwa wazee.
Pichani
juu na chini ni washiriki wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye
semina ya Fursa na wengine waliweza kuandika jambo lolote waliloliona
lina manufaa kwao.
Sehemu ya Washirikiwa semina ya Fursa wakiwa ndani ya ukumbi wa Chuo cha TAKE wakifautilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo .
Mtangazaji
wa Clouds FM kupitia kipindi cha Jahazi,Mdau Mussa akizungumza na
wakazi wa mjii wa Tabora waliofika kwenye semina ya Fursa,iliyofanyika
kwenye ukumbi wa chuo cha TEKU mjini Tabora.
Baadhii ya Washiriki wakitoka nje ya ukumbi baada ya semina ya Fursa kuisha
0 comments:
Post a Comment