Friday 5 September 2014

Basi la J4 Express  T677 CYC lililokuwa linatoka Sirari kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi la Mwanza Coach T736 AWJ lililokuwa likitoka Mwanza kwenda Musoma leo asubuhi.
 Ajali hiyo  imetokea katika eneo la daraja la sabasaba, Musoma na habari ambazo hazijathibitishwa zinasema zaidi ya watu 50 wamefariki katika ajali hiyo na wengine wakijeruhiwa vibaya,Tamasha la Fiesta lililokuwa lifanyika leo kwenye uwanja wa Karume limeahirishwa baada ya ajali hiyo amesema Mkurugenzi wa Maendeleo na Utafiti wa  Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba.
Ameongeza kwamba wafanyakazi wote wataungana na waombelezaji pamoja na wananchi wote wa Musoma ili kutoa msaada pale utakapohitajika lakini pia kuomboleza pamoja na wana Musoma kufuatia ajali hiyo mbaya, Endelea kufuatiliataarifa zaidi za ajali hiyo .
 
Baadhi ya maiti zikiwa zimelazwa chini baada ya kunasuliwa kwenye mabasi hayo
 

0 comments:

Post a Comment