Kwa maoni yangu, kikao kati ya Rais Jakaya Kikwete na Wapinzani wakiwemo UKAWA, kinastahili pongezi na sio kubezwa, na huu ukimya wa matokeo ya kikao hicho, ni Ukimya Dawa!, yaani "silence is golden!".
Kuna msemo unaosema "No News, is Good News!", na "Kimya Kingi Kina Mshindo Mkuu!", tangu jana Rais JK alipokutana na Wapinzani kupitia TCD na miongoni mwao wakiwemo wana UKAWA, kumekuwepo na ukimya, unaopelekea kuzua speculations hizi na zile kuhusiana na matokeo ya kikao hicho, hali inayopekea wale wabunifu wa mambo kuanza kubuni au matokea hasi au matokeo chanya!.
Mtu yoyote anapokamatwa na polisi, duniani kote, kitu cha kwanza anachoelezwa ni kwa polisi kujitambulisha na kumweleza mhusika kuwa "Uko Chini ya Ulinzi" "You have the right to remain silance!" "anyathing you say, may be used for or against you before the court of law!" wakimaanisha unaruhusiwa kukaa kimya na chochote utakachosema kinaweza kutumika kama ushahidi mahakama kukuokoa au kukuangamiza!. Hivyo ukimya nao ni jibu tosha!.
Naomba tuchukue fursa hii kupongeza uwepo tuu wa kikao hicho regardless ya matokeo yoyote!, ile kukubali tuu, kukutana, kukaa na kuzungumza ni dawa tosha ya kutibu ule mkwamo wa maridhiano katika mchakato wa katiba!.
Hata mgonjwa anapokwenda kwa daktari, ile kuzungumza tuu na daktari kuhusu ugonjwa wake, ni tiba tosha ya ugonjwa huo kabla hata ya dozi kuanza kutolewa!. Hivyo uwepo wa kikao hiki unastahili pongezi na sio ridicule!.
0 comments:
Post a Comment