Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya
watoto wanaotumikishwa Duniani inafikia milioni 169 kati ya hao wapo
wenye umri wa miaka mitano, wanaotoka katika familia maskini ambao
hulazimika kufanya kazi ili waweze kuishi na hivyo kukoa fursa ya upata
elimu na malezi bora.
Kwa upande wa Tanzania asilimia
27.5 ya watoto wenye umri wa chini ya miaka 17 wanatumikishwa katika
ajira hatarishi zikiwemo za kufanya kazi majumbani, sehemu za starehe,
uvuvi, migodini, mashamba ya tumbaku na machungwa.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na
Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete wakati wa
hafla ya chakula cha jioni kilichoandalia kwa ajili ya kampeni ya
kupambana na utumikishwaji wa watoto iliyoandaliwa na International
Rescue Committee (IRC) na kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar
es Salaam.
Mama Kikwete ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema
utumikishwaji wa mtoto ni hali inayomkosesha mtoto haki zake za msingi
kama vile elimu, afya, malezi na kutokupata nafasi ya kucheza na watoto
wenzake.
“Utumikishwaji wa mtoto unamadhara
makubwa kwa mtoto mwenyewe, familia, jamii na taifa kwa ujumla. Kitendo
hiki humsababishia mtoto kuathirika kiakili,kiafya
kisaikolojia,kimakuzi na hata katika mazingira mengine hupelekea kifo
chake”.
Pia husababisha umaskini kati ya
kizazi hadi kizai, na hivyo kudidimiza maendeleo ya Taifa. Aidha mtoto
anayetumikishwa hukosa ndoto za maisha bora kwa siku za usoni kwa kuwa
alikosa fursa hiyo akiwa mdogo.
Mwenyekiti huyo wa WAMA alisema
mazingira mazuri ya kisera na kisheria yametayarishwa kwa ajili ya
kuwalinda watoto dhidi ya unyanyasaji ukiwemo wa utumikishwaji katika
ajira hatarishi kinachotakiwa ni juhudi za pamoja ili kuhakikisha watoto
hawatumikishwi katika jamii.
Akimkaribisha Mama Kikwete ili
aweze kuongea na wageni waliohudhuria hafla hiyo Mkurugenzi wa IRC
Tanzania Elijah Okeyo alisema Ili kukabiliana na tatizo la ajira za
watoto mwishoni mwa mwaka 2012 Serikali ya Marekani kupitia idara ya
Kazi iliwapatia dola milioni 10 kwa ajii ya mradi wa WEKEZA ambao
unafanya kazi zake katika wilaya sita zilizopo katika mikoa ya Tanga na
Kigoma.
Kupitia mradi huo watoto 15,000
walitoka katika ajira hizo, walilindwa ili wasiweze kujihusha na ajira
za watoto na kuweza kurudi shuleni kuendelea na masomo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa IRC
wa Kanda ya Afrika ya Mashariki na Pembe ya Afrika Kurt Tjossem alisema
kazi ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ni ya
kila mtu na siyo ya mtu mmoja hivyo bsi wadau wote wa watoto waendelee
kuwekeza katika elimu kwani ndiyo ukombozi wa maisha ya mtoto.
Alisema inasikitisha kuona mtoto
anaacha shule na kwenda kufanya kazi ili aweze kuongeza kipato cha
familia hali hiyo siyo kama inawaweka mbali na utoto wao bali
inawaharibia maisha yao ya baadaye lakini kuna matumaini kwao ambayo
yataanzia kwa jamii yao lakini ili waweze kufanikiwa ni lazima wadau
wote wawaunge mkono
Licha ya kufanya kazi zake hapa
nchini IRC pia inafanya kazi katika nchi 40 za kuokoa maisha, kuwasadia
watu ili waweze kujenga upya maisha yao, kuwalinda watu ambao maisha
yao yameathiriwa na vita pamoja na majanga ya asili.
0 comments:
Post a Comment