Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa CARMATEC
Ndugu Elifariji Makongoro mara baada ya kuwasili kwenye Kijiji cha Kondo
kilichoko katika kata ya Zinga wilayani Bagamoyo kushiriki katika siku
ya kitaifa ya biogas iliyofanyika kijijini hapo na Mama Salma akiwa
mgeni rasmi tarehe 10.9.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akitembelea maonesho ya biogas yaliyofanyika
katika Kijiji cha Kondo tarehe 10.9.2014. Mkurugenzi Mkuu wa CARMATEC
Ndugu Elifariji Makongoro (kulia) akimpatia maelezo mbalimbali ya kazi
zinazofanywa na shirika hilo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Mheshimiwa Mwantumu Mahiza.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha wageni mara
baada ya kuwasili Kijijini Kondo kwenye sherehe za kilele cha siku ya
biogas kitaifa.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe huku akishirikiana na viongozi
mbalimbali ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa mtambo wa wa 10,000 wa
Biogas hapa nchini. Mtambo huo unaomilikiwa na Ndugu Bakari Seif na
Mkewe Mwanaidi Said (wa pili na wa tatu kutoka kushoto). Wa kwanza
kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Ndugu Eliakim
Maswi, kulia kwa Mama Salma ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Ndugu Mwantumu
Mahizana. Aliyesimama kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kondo Ndugu
Ramadhan Seleman akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa CARMATEC Ndugu
Elifariji Makomgoro.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu
wa CARMATEC Ndugu Elifariji Makongoro kuhusu ujenzi wa mtambo huo na
unavyofanya kazi.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akizungumza na wageni waalikwa na mamia ya wananchi
waqliohudhuria sherehe ya siku ya biogas kitaifa iliyofanyika katika
Kijiji cha Kondo huko Bagamoyo tarehe 10.9.2014.
0 comments:
Post a Comment