Sunday 14 September 2014




TANZANIA mwakani itaingia kwenye Uchaguzi Mkuu 2015, rais atakayeingia madarakani kuiongoza nchi atajulikana hapo huku tayari baadhi ya wanasiasa wametangaza nia ya kugombea, wengine wanatajwatajwa kufanya hivyo.

Baadhi ya viongozi wanaotabiriwa na Mastaa wa Bongo Movie kuwa marais kwenye Uchaguzi Mkuu 2015
Sasa kuelekea uchaguzi huo ambao pia utajumuisha ubunge na udiwani, baadhi ya mastaa Bongo wamefunguka kuhusiana na nani wanayempenda awe rais katika kinyang’anyiro hicho.Wafuatao ni baadhi ya mastaa ambao walizungumza juzi na Risasi Jumamosi wakiweka wazi nani wanamkubali kuiongoza Bongo baada ya Rais Jakaya Kikwete ‘JK’ kumaliza muda wake.GPL(P.T)
Kulwa Kikumba ‘Dude’;
“Mimi kwangu zaidi ya wote ni Mizengo Pinda (waziri mkuu). Huyu ndiye chaguo langu kwa kweli.”
Yobnesh Yusuph ‘Batuli’;
“Mimi sina mengi ya kuongea ila natamani Bernard Camillius Membe (waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa, CCM) awe rais wa nchi hii, nitafurahi sana Mungu akijalia hivyo.”

Baadhi ya mastaa wa kike waliotabiri viongozi.
Abdul Sykes ‘Dully Sykes’;
“Dah! Umeniuliza swali la msingi sana, kama ulikuwepo kwenye ndoto zangu kwani nilikuwa natafuta wapi pa kusemea. Unajua Lowassa ni rafiki wa Kikwete, pili ni mpambanaji mzuri, tatu ni ‘brazamen’ mwenzetu. Anafaa kuwa prezdaa!”
Esha Sali Buheti;
Kwa upande wake, Esha alisema achana kabisa na Lowassa kwani ndiyo tumaini la wanyonge wote wa nchi hii.
Issa Musa ‘Cloud 112’;
“Kiukweli mimi hadi sasa niko njia panda kati ya hawa watu wawili, Lowassa na Membe kwani wote wana faida kubwa kwangu, ukija katika suala zima la kazi yangu Membe amenisaidia sana.
“Vilevile Lowassa ametoa mchango mkubwa sana katika sanaa hapa nchini lakini kubwa zaidi na linalonisuuza roho yangu ni pale ukiachana na imani yake ya Ukristo lakini anasaidia hata Waislam, aliwahi kusimamia vitabu vya Shehe Mkuu wa Tanzania, Isa Bin Simba.”
Jacqueline Wolper ‘Jack’;
“Membe na Lowassa mmh! Hapa niache kwanza nifikirie. Lakini Lowassa da! Anyway, ngoja nifikirie kwanza.”

Baadhi ya mastaa wa kiume.
Steven Mengele ‘Steve Nyerere’;
Huyu hakupatikana mwenyewe kumtaja mtu anayemwona anafaa kuwa rais, lakini watu walio karibu naye wanadai yupo upande wa Membe, wengine wanasema anamkubali Lowassa.
Kwa upande wake Mahsein Awadhi ‘DK Cheni na Wema Sepetu licha ya kutokupatikana hewani lakini wanatajwa kuwa upande wa Lowassa.
Mbali na waliotajwa na mastaa hao, wengine ambao wanadaiwa kugombea urais mwakani ni Hamis Andrea Kigwangalla (Mbunge wa Nzega, CCM) na January Yusuf Makamba (naibu waziri wa sayansi na teknolojia na Mbunge wa Bumbuli, CCM). Hawa wametangaza nia.Wengine ni Samuel John Sitta, John Pombe Magufuli, William Mganga Ngeleja na Steven Masatu Wassira. Hawa wanatajwatajwa, hawajatangaza nia.

0 comments:

Post a Comment