Tuesday, 23 September 2014
03:41
Unknown
Mbunge wa jimbo la Temeke na
Mwenyekiti wa Wabunge Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu akiwa anaingia
Ofisi ya katibu kata,ya chama cha Mapinduzi CCM Buza Dar es Salaam
Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti
wa Wabunge Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu akitia saini katika
kitabu cha wageni Ofisi ya katibu kata ya chama cha Mapinduzi CCM Buza
Dar es Salaam.
Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti
wa Wabunge Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu,(wapili kulia) wakipiga
makofi wakiimba wimbo wa chama hicho mara alipo wasili Ofisini
hapo,kuanzia kushoto ni Mwenyekiti UVCCM kata ya Buza,Mwenyekiti wa
Umoja wa Vijana Jimbo la Temeke na msaidizi wa Mbunge wa jimbo hilo
upande wa Vijana.Peter Sillo,aliye vaa shati la kijani ni Mwenyekiti wa
CCM kata ya Buza, Shabani Bambo na wakwanza ni Katibu kata ya Buza
Shabani Abdallah.
Katibu kata ya Buza Shabani Abdallah,
akimkaribisha Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu, na
akitambulisha katika hafla fupi ya kukabidhi jezi na pesa taslim kwa
matumizi mbalimbali ya kiofisi, katika moja ya ahadi aliyoitowa kwa
majimbo matano kwa wanachama wa chama cha Mapinduzi(CCM) Buza.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Temeke (CCM),Ally Mehalla ,akisalimia wanachama wa chama hicho
msaidizi wa Mbunge wa jimbo la Temeke
upande wa Vijana.Peter Sillo kushoto akisalimia wanachama wa chama cha
Mapinduzi (kushoto) Mwenyekiti wa( CCM) kata ya Buza, Shabani Bambo
anaye fatia ni Mbunge wa jimbo la Temeke Abbas Mtemvu na kulia ni Katibu
kata ya Buza Shabani Abdallah.
Viongozi wa Matawi kata ya Buza
Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti
wa Wabunge Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu(kulia), akikabidhi Pesa
Taslim kwa katibu wa Uchumi wa chama hicho Hawa Zuberi, kwa matumizi
mbalimbali ya kata ya Chungu Buza Dar es Salaam.
Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti
wa Wabunge Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu(kulia) akimkabidhi Jezi na
pesa taslim katibu wa Tawi la Mashine ya Maji5 Baraka Mohamedi
Mbunge wa Jimbo la Temeke na Mwenyekiti
wa Wabunge Mkoa wa Dar es salaam,Abbas Mtemvu (kulia),akimkabidhi
Mwenyekiti wa CCM kata ya Buza seti ya Jezi pamoja na Pesa taslim
Sh.milioni moja na laki moja. Johari Mkonde (kushoto), kati ya ahadi
aliyoitowa kwa majimbo matano kwa wanachama wa chama cha Mapinduzi .
anaye shuhudia ni Mwenyekiti wa chama hicho kata ya buza, Shabani Bambo.
Mbunge wa Jimbo la Temeke akitoka na
viongozi kwanda eneo lililo haribiwa na Mvua na kusababisha njia hiyo
kutopitika na Magari yakawa hayapiti katika njia hiyo, kati ya Vituka
Machimbo na Buza Shule na jinsikani wataweza kuweka Daraja katika Mto wa
Buza ili wanafunzi na wananchi waweze pita kwa urahisi kutokana na
ukaribu wa eneo hilo.
Wakiwa katika kituo kidogo cha Polisi
cha Buza ,kujionea maendeleya ya kituo hicho baada ya kutoa Pesa awamu
ya kwanza na kuahidi kukimalizia na kuwawekea Fenicha mbalimbali kituoni
hapo.
Njia iliyo haribiwa na Mvua na Gari kuto pita tena
Monday, 22 September 2014
22:09
Unknown
Warembo
15 kati ya 30 wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2014
wakisindikizwa na mkali wa Bongo Fleva kutoka Jijini Dar es Salaam,
Tunda Man, wametoa burudani kali wakati wa shindano dogo la awali la
kumtafuta mrembo mwenye kipaji lililofanyika Babati Mkoani Manyara.
Pichani juu ni washindi wa tano waliofanikiwa kuingia fainali ya
shindano hilo la vipaji litakalofanyika jijini Dar es Salaam baada ya
wengine 15 kufanyika Arusha mjini.
Warembo hao walishindana vikali katika kucheza na kuimba miziki ya aina mbalimbali.
Jopo la majaji likifuatilia kwa makini shindano hilo
Kila aina ya stile za uchezaji zilioneshwa na warembo hao jukwaani…
wadau wa sanaa ya Urembo Babati wakifuatilia shindano hilo.
Mkuu
wa Wilaya ya Hanang, Christina Mndeme aliye mwakilisha Mkuu wa Mkoa wa
Manyara, akiwa na waratibu wa show hiyo, Mzee Ally Sumaye (kushoto) na
Mfanyabiashara Mohamad Bajwa.
Msanii wa Bongo Fleva Tunda Man akitoa burudani kwa wadau wa urembo Babati.
Friday, 19 September 2014
13:10
Unknown
BAADA ya siku
chache kupita kufuatia tukio la nani amefanya kitendo kiovu cha kurusha bomu la
kienyeji katika mtaa wa Msufini Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, na kujeruhi
baadhi ya askari Polisi mjini hapa, Mkuu wa mkoa huo Said Mwambungu amekutana
na waendesha pikipiki wa manispaa hiyo na kuwataka kujenga ushirikiano
ili kuweza kulinda amani ya nchi dhidi ya maadui ambao hawalitakii mema taifa hili.
Mwambungu
amekutana leo na madereva hao maarufu kwa jina la “Boda boda” katika ukumbi wa
Songea Club uliopo mjini Songea, akisisitiza kujenga ushirikiano kwa vyombo vya
usalama ili kuweza kupata ukweli wa tukio hilo na kuwafanya wakazi wa mji huo,
watu wengine (wageni) wanaoingia na kutoka kuondoa hofu na kuishi katika hali
ya usalama.
Akizungumza kwa
njia ya simu na mwandishi wa habari hizi, Mkuu huyo wa mkoa alisisitiza kuwa
jamii ihakikishe kwamba amani utulivu vinatawala miongoni mwao, na pale wanapoona
kuna sintofahamu ni vyema watoe taarifa katika vyombo husika vya usalama ili
kuweza kubaini uhalifu unaofanyika na hatua ziweze kuchukuliwa haraka dhidi ya
wahalifu.
“Ni kweli leo
nimezungumza nao, ni kawaida yangu kukutana nao jambo kuu nimesisitiza kujenga
ushirikiano na amani, na waache kutumiwa katika mambo ya kisiasa, siku
zote amani ndio msingi mkuu”, alisema Mwambungu.
Mwambungu
aliongeza kuwa hivi sasa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea na uchunguzi
juu ya tukio hilo, na kwamba mpaka sasa hakuna mtu aliyepatikana ambaye
anahusika kutenda unyama huo.
Pamoja na mambo
mengine tukio la kurushwa kwa bomu hilo, lilitokea Septemba 16 mwaka huu majira
ya 1:25 usiku katika mtaa wa Msufini katika Manispaa ya Songea na kuwajeruhi
askari Polisi watatu kati ya w anne waliokuwa doria huku Jeshi la Polisi nchini
likithibitisha kuwa bomu hilo limetengenezwa kienyeji.
Askari
waliojeruhiwa ni G 5515 PC John, G 7351 PC Ramadhan na WP 10399 Felista ambapo
baada ya kujeruhiwa kwa bomu hilo, walikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya
mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya matibabu zaidi.
PC John aliyepata majeraha kiasi alipatiwa matibabu siku hiyo na kuruhusiwa, huku askari wawili PC Ramadhan na WP Felista wakiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.
PC John aliyepata majeraha kiasi alipatiwa matibabu siku hiyo na kuruhusiwa, huku askari wawili PC Ramadhan na WP Felista wakiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.
Subscribe to:
Posts (Atom)