Monday, 22 December 2014


1q
Rais Dr Jakaya Kikwete amemuachisha kazi waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo  Makazi Profesa Anna Tibaijuka kutokana na tuhuma za kupata mgao wa Fedha za Akaunti ya Escrow kiasi cha bilioni Moja na Milioni Mia Sita ambazo alidai amepewa mchango kwa ajili ya shule, Rais Jakaya amesema Tumeamua mwenzetu huyu atupishe ili tuchague mtu mwingine wa kuhudumu katika wizara hiyo kutokana na maswali magumu.
Akiwa kama Mtumishi wa serikali ambaye anatakiwa kufuata maadili ya Utumishi  wa umma  aliamua kupokea kiasi kikubwa cha fedha huku akijua kimaadili kama mtumishi wa serikali haitakiwi, Rais Dr. Jakaya Kikwete amesema hayo wakati  akizungumza na taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa Wiazara hiyo Eliackhim  Maswi  amesema ameagiza uchunguzi ufanyika na katika muda wa siku mbili au tatu hivi atapewa taarifa ya uchunguzi huo na kuchukua hatua stahiki.
Na Kwa upande wa Majaji wa Mahakama Kuu waliotuhumiwa Rais Dr. Jakaya Kikwete amesema anamwachia Jaji Mkuu Mh. Jaji Mohammed Chande Othman ili achukue hatua za kimaadili kutokana na taratibu za kimahamama na mara baada ya kujiridhisha atapewa taarifa na Jaji mkuu na kuchukua hatua.

0 comments:

Post a Comment