Thursday, 18 December 2014


wabunge wakiwa katika vikao bungeni 
 
Wabunge wa Kenya wametofautiana vikali bungeni na kuvuana mashati huku wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswada tatanishi wa usalama ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa wakenya.
Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.
Wabunge wa upinzani walipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo.
Seneta Johnston Muthama alijipata pabaya kwani long'i yake iliraruliwa katika mvutano bungeni humo 
Mwenyekiti wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kuyaja mabadiliko yaliyopendekezwa kufanyiwa mswada huo lakini wabunge walianza kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada huo wakisema 'bado mapambano.'
Spika wa bunge Justin Muturi wakati mmoja aliamuru walinzi wa bunge kuwaondoa baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa mjhadala ambao ulitarajiwa kuwa kaa moto, hasa kw aupande wa upinzani.
Mswada huo ambao umewasilishwa bunge kufuatia matukio ya utovu wa usalama na mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwaw augaidi wanaweza kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya uchunguzi.

0 comments:

Post a Comment