Tuesday 2 June 2015













Habari  Zilizopo  Katika  Magazeti  ya  Leo  Jumatano  ya  Tarehe  3 Juni 2015


Vumbi la kinyang’anyiro cha uteuzi wa kuwania urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), linaanza rasmi Dodoma leo kwa wanachama wake watano kuchukua fomu wakiomba uteuzi huo.
 
CCM imepanga kuanzia leo Juni 3 hadi Julai 2, mwaka huu, kuwa siku za kuchukua na kurudisha fomu za wanachama wake wanaoomba uteuzi kuwania urais.
 
Uteuzi huo ni kwa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini kwa uteuzi wa Rais wa Zanzibar, fomu zitakuwa zikitolewa kisiwani Unguja.
 
Tayari wanachama wa CCM kadhaa wamekwisha kutangaza nia ya kumrithi Rais Jakaya Kikwete huku wengine zaidi wakitarajiwa kufanya hivyo.
 
Kwa mujibu wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) wa Oganaizesheni, Dk Muhammed Seif Khatib, uchukuaji wa fomu hizo unaanza rasmi leo.
 
Khatib aliwaambia waandishi wa habari jana katika Makao Makuu ya CCM ‘White House’, Mtaa wa Nyerere mjini Dodoma  kuwa fomu zitaanza kutolewa saa nne asubuhi.
 
Alisema kwa mujibu wa orodha waliyonayo, wanachama watano watachukua fomu hizo kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 10:30 jioni, na kila mmoja amepewa saa moja na wametenga muda wa kuzungumza na waandishi wa habari kwa wagombea ambao wataona inafaa kwao.
 
“Uchukuaji huu wa fomu haukufuata umaarufu wa mtu, ujuzi, alfabeti, nafasi yake katika Chama na Serikali, bali umefuata aliyewahi kutoa taarifa kwa Chama,” alisema Khatib akifafanua uchukuaji huo.
 
Alimtaja wa kwanza kuchukua fomu kuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya kuanzia saa 4 kamili hadi saa 5:30.
 
Profesa Mwandosya atafuatiwa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wassira kuanzia saa 5:30 na atafuata Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa atachukua fomu kuanzia saa saba kamili.
 
Wa nne atakuwa Waziri wa zamani wa Muungano, Balozi Amina Salum Ali kuanzia saa 8:30 mchana na pazia la ufunguzi litafungwa saa 9:30 alasiri na mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Charles Makongoro Nyerere.
 
Mbali ya wanachama hao watano, wanaCCM wengine ambao wametangaza nia ya kuwania urais ni Lazaro Nyalandu, Frederick Sumaye, Profesa Sospeter Muhongo, January Makamba, Mwigulu Nchemba na Luhaga Mpina.
 
Wanaotajwa ni pamoja Bernard Membe, William Ngeleja, Dk Titus Kamani, Luhaga Mpina, Mizengo Pinda, Dk Asha-Rose Migiro, Shamsi Vuai Nahodha, Dk Emmanuel Nchimbi na Dk Hamis Kigwangalla.
 
Katibu huyo wa Oganaizesheni alisema uchukuaji huo wa fomu utazingatia taratibu zilizowekwa na CCM na kutakuwa na fomu tatu zitakazopewa wagombea.
 
Fomu ya kwanza itahusu maelezo binafsi ya mgombea, itahusu uzoefu na ujuzi wake, nyingine itakuwa ya kujaza orodha ya wadhamini wake na nyingine ya masharti kama yalivyokubaliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa,” alifafanua Dk Khatib.
 
Alisema katika wadhamini, mgombea atatakiwa kupata wadhamini 450 kutoka katika mikoa 15 ya Tanzania Bara na mikoa mingine mitatu ya Tanzania Zanzibar.
 
“Mjumbe yeyote wa Mkutano Mkuu wa Taifa haruhusiwi kumdhamini mgombea, pia mwanachama haruhusiwi kudhamini mgombea zaidi ya mmoja,” alifafanua.
 
Alisema ili kuonesha uhalali wa fomu hizo za wadhamini, zitapaswa kuwa na mhuri wa Katibu wa CCM wa wilaya husika pamoja na saini yake na pia mdhamini atapaswa kusaini na kuandika kadi yake ya uanachama.
 
Alisema wagombea hao watakapofika kuchukua fomu, wanapaswa kuwa na ada ya Sh milioni moja na watasaini daftari maalumu kuonesha ndio waliochukua fomu.
 
“Tumepanga muda wa saa moja moja na nusu kwa kila mgombea kuwapo hapa. Na akishachukua fomu tumepanga anayetaka azungumze na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa NEC,” alisema Dk Khatib.
 
Alisema katika chumba cha uchukuaji wa fomu, wataruhusiwa mgombea kuingia na watu wasiozidi 10.
 
 “Katika chumba hiki (cha mikutano na waandishi katika Makao Makuu) tutaruhusu mgombea kuingia na watu wasiozidi 10… mkewe na jamaa zake wengine, wanaomsindikiza, sijui wengine mnawaita wapambe, mimi nawaita wanaomsindikiza,” alisema Katibu huyo.
 
Aliwataka wagombea wengine wanaotaka kuchukua fomu hizo kuwasiliana mapema na ofisi yao kwani alisema wangependa kazi ya uchukuaji fomu kudumu kwa siku zisizozidi tano ili shughuli nyingine ziendelee.
 
“Tunawaomba wagombea wengine wanaotaka kuja kuchukua fomu kufanya hivyo mapema. Tungependa ndani ya siku tano tuwe tumemaliza ili shughuli nyingine ziendelee kwani hata wao wana kazi ya kutafuta wadhamini mikoani,” alifafanua kiongozi huyo mkongwe

Sunday 31 May 2015


NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, amesema kwa sasa nchi ipo njia panda, hivyo kuna haja ya kutumia busara ili kuchagua kiongozi atakayeleta maendeleo.
 
Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki , wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Tawi la Mwenge, kuhusu utandawazi na maendeleo ya jamii.
 
January, Mbunge wa Bumbuli, ambaye pia ametangaza kutaka kugombea urais, alisema Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu ni muhimu kuliko zote, kutokana na wananchi kuwa njia panda ambayo moja ina mashimo na nyingine ina mafanikio.
 
Alisema matamko mbalimbali ya viongozi wa dini katika sherehe za sikukuu na mwaka mpya yanaonyesha nchi ipo njia panda kutokana na wananchi kukosa amani ya moyo.

“Uchaguzi huu una majaribu mengi, kuna viongozi wanafanya kazi ya kutoleana lugha kali na kushutumiana wizi, tafadhali angalieni uchaguzi huu ni muhimu na tunaweza tukachagua watu watakatuingiza shimoni ama watakaoweza kutupeleka katika mafanikio,” alisema January.
 
Alisema hiki ni kipindi cha tatu ambacho Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaingia katika uchaguzi wa ndani, hivyo anaamini bado kinaendelea kujifunza katika masuala hayo.
 
Alisema kuna mambo yanaonyesha wazi kuwa katika kipindi hiki nchi inajaribiwa,  hivyo busara za viongozi zinahitajika ili kuweza kuivusha nchi salama na watu waishi vizuri baada ya uchaguzi.
 
Alisema vijana pia wana nafasi kubwa ya kupaza sauti ili kupata viongozi bora, ikiwa pamoja na kuuliza maswali kuhusu hatima ya nchi badala ya kushabikia.
 
Mmoja wa wanafunzi alimuuliza endapo atakuwa rais atafanya nini ili Ikulu isiwe pango la walanguzi, lakini alijibu hawezi kuongelea masuala ya siasa katika eneo la taaluma.
 
“Nisingependa katika mazungumzo haya kusema nitafanya nini nikichaguliwa ili mnichague, swali linaloelekeza huko sitojibu, tusifanye siasa kwa sababu hii ni sehemu ya taaluma, kama unataka mambo hayo nitafute mtaani au katika mitandao,” alisema January.
 
Pia aliitaka Tume ya Uchaguzi (NEC) kuharakisha mchakato wa uandikishaji wapiga kura ili kuhakikisha watu wanapata haki ya kupiga kura.
 
Alisema hatafurahi kuona mtu anashindwa kupiga kura kwa sababu za kutojiandikisha, badala yake asiyepiga kura awe ni kwa sababu zake binafsi.


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Kaskazini, kimemchagua Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Godbless Lema, kama Kamanda wa Operesheni ya Uandikishaji wa Daftari la Wapigakura katika kanda hiyo.
 
Hayo yalisemwa juzi jijini hapa na Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Calist Lazaro, alipokuwa akizungumza  katika kikao maalumu cha mkakati  kilichowashirikisha viongozi wa Wilaya ya Arusha, wenyeviti wa kata na viongozi wa Chadema wa Serikali za Mitaa kutoka kata 25 za Jiji la Arusha.

“Tuweke akili zetu kwenye BVR kwani hakuna ushindi bila watu kujiandikisha, naomba nimtambulishe Lema kama Kamanda wa Operesheni ya BVR katika Kanda ya Kaskazini, ambaye ataongoza kampeni hiyo ya kuhamasisha wananchi wajiandikishe kwa wingi ili tuweze kushinda,”alisema Lazaro
 
Alisema kutokana na uhamasishaji wa Lema ambaye pia ni Mbunge wa Arusha Mjini, utakiswezesha chama hicho kushinda katika uchaguzi mkuu na hata kuongeza idadi ya majimbi kutoka mawili ya sasa.
 
Awali Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Arusha, Derick Magoma, alisema lengo la kikao hicho ni mkakati ya kuhimiza wananchi kujiandikisha kwenye daftari hilo ili kushinda katika uchaguzi huo kwa kishindo.
 
“Tusipojiandaa sasamhatutaweza kushinda uchaguzi huu,kwani tumedhamiria kushinda kwa kishindo, ndiyo maana tumeitana hapa kupanga mikakati ya ushindi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kujiandikisha, mwaka huu hata walete magari yenye maji ya kuwasha, mabomu, lakini ushindi ni lazima,”alisema
SOURCE MPEKUZI
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )













SOURCE MPEKUZI

Sasa  ni  zamu  ya  Mwigulu  Nchemba  kutangaza  nia  ambapo tayari amewasili katika ukumbi wa Mwl. Nyerere katika chuo cha mipango Dodoma ili kutangaza   nia  yake  ya  kugombea  Urais  kwa  tiketi  ya  Chama  cha  Mapinduzi, CCM.
Hapa  nimekuandikia  pointi  muhimu  anazotoa  Mwigulu Nchemba (Zinaanzia  chini  kuja  juu);
25: Mh. Mwigulu tayari amemaliza kuzungumza na sasa anaendelea kufurahi na watu walioko ukumbini. Kinachofuata  kwa  sasa  ni  maswali  mbalimbali  ambayo  ataulizwa  na  kuyajibu.

24: Mambo matatu ninayowaomba Watanzania ni kwamba mniamini, pili mniunge mkono na tatu nitawavusha. 

23: Natangaza rasmi kuomba ridhaa ya kugombea katika chama changu ili niweze kuleta mabadiliko Katika Nchi yangu. 
 
22: Napoenda kupigana vita hii siendi kupigana kwaajili ya Watanzania ila mimi mwenyewe maana umaskini unanigusa.

21: Ukiwaondoa vijana mjini wakati wakifanya kazi halali kwa kigezo cha uchafu,watarudi mjini na kufanya kazi haramu.
 
20: Tunaposimamia kuacha kufanya kazi kwa mazoea ndio tunasema mabadiliko ni vitendo na wakati ni sasa. 

19: Ninapotangaza nia ya jambo hili nimetathimini vya kutosha na nikajiridhisha na ahadi yangu ni kwamba nitawavusha.

 
18: Nawaambieni nawaomba kazi hii nikiwa bado nina nguvu ili niweze kufika mwenyewe maeneo yenye migogoro ya ardhi.
 
17: Tutasimamia Muungano wetu maana sio wa vitu ila ni watu. tutahakikisha uchumi wa Zanzibar nao unapewa kipaumbele.
 
16: Mtu anayeiba dawa ambazo zingemtibu maskini huyo ni mhujumu, tutamnyang'anya leseni yake na atakwenda jela.
 
15: Ninaposema kukomesha rushwa nitazingatia maslahi ya Wafanyakazi, haiwezekani wengine Wale kidogo na wengine kubwa .
 
14: Mtu anabakiza muda mchache hadi anakuja kustaafu unamuongezea muda tena kazini wakati kuna vijana wasio na kazi.
 
13: Mtu yoyote akithibitika amefanya vitendo vya rushwa, atafilisiwa, atafukuzwa kazi na atafungwa.
 
12: Rushwa hupofusha macho ya wenye akili na rushwa hurudisha nyuma maendeleo.
 
11: Awamu ya 5 nataka kuona nchi ikiingia kwenye uchumi wa viwanda na vijana wakifanya kazi kwa shift usiku na mchana .
 
10: Pia jambo lingine la kuzingatia ni Udhibiti wa matumizi mabaya ya fedha na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. 

9:Mambo ya kuzingatia ni Kila mtu kulipa kodi anayostahili na sio kukandamiza wafanyakazi na kinamama wauza vitumbua .

8:Mkataba wa Rais wa awamu ya tano ni juu kazi anazoenda kufanya na sio kazi alizowahi kufanya.  


7: Faida  ya  kuwa  kiongozi  Kijana  ni  kuwa Unafanya kazi ukiwa na nguvu na ukimaliza unapumzika, kwahiyo unajiuliza tena hilo?
 
6: Kiongozi akipatikana kwa mazoea, atafanya kazi kwa mazoea. Nawaambieni tunataka tukomeshe kufanya kazi kwa mazoea

5: Kukaa sana serikalini si kigezo, unaweza kukaa sana serikalini na ukawa umesababishia hasara kubwa Taifa hili.


4: Nilipomaliza shahada ya 2  nilibeba zege na mke wangu alipika mama ntilie, natambua tatizo la ajira kwa vijana.

3: Kiongozi aliyekaa muda mrefu madarakani maana yake ni kwamba amesahau shida za wananchi. 

2: Nimeamua kutangazia nia Dodoma kwakuwa ni Makao makuu ya Nchi na pia makao makuu ya chama.
 
1: Namshukuru MUNGU kwa kuniwezesha leo kusimama mbele yenu kwaajili ya kutangaza jambo kubwa kwaajili ya nchi yetu .
Source Mpekuzi
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

  1. Nianze kwa kutoa shukrani kwenu wote mlioacha shughuli zenu ili kuja hapa kunisikiliza. Kuja kwenu hapa kwa wingi ni ishara ya imani mliyonayo kwangu, Nawashukuru sana

  2. Kwa zaidi ya mwaka mzima, kumekuwepo na miningo’no kuhusu uwezekano wangu kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Aidha kutokana na mijadala ya wananchi au kupitia mitandao ya kijamii au vyombo rasmi vya habari, mining’ono hiyo imefanya baadhi ya watu wanifuate ili wanishauri nigombee na wengine wamenipigia simu kwa kunishawishi nisisite kugombea

  3. Leo, nakuja hapa Mwanza kuvunja ukimya na kumaliza minong’ono kwa kutangaza rasmi kwamba nimekata shauri kugombea nafasi ya urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
KWANINI NAGOMBEA
Zikosababu kadhaa, ambazo zimenisukuma kugombea kufikia uamuzi huo
  • Haki yangu ya kikatiba. Hii ni sababu ya msingi lakini siyo yenye uzito, kwa vile ni haki ya kikatiba na ni kwa ajili ya watanzania wote. Hivyo zinahitajika sababu za ziada licha ya haki ya kikatiba

  • Naifahamu Tanzania, Kwa muda mrefu tangu miaka ya 1970 nimeshirikishwa katika uongozi wa nchi yetu tangu nikiwa na umri wa miaka wa 27
  • 1970 kwa mara ya kwanza nilichaguliwa kuwa mbunge wa Mwibara katika wilaya ya Bunda

  • 1973 niliteuliwa kuwa waziri mdogo (Juniour Minister)
  • 1975 Niliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na katibu wa TANU wa mkoa
  • 1982-1985 Afisa mwandamizi mkuu ubalozi wa Tanzania Marekani

  • 1987-1989 Raisi alniteua kuwa naibu waziri wa serikali za mitaa na mifugo na vyama vya ushirika
  • 1989-1990 Niliteuliwa kuwa Waziri wa kilimo, mifugo

  • 1990-1991 Mkuu wa mkoa wa pwani na katibu wa CCM Mkoa

  • 2005-2015 Waziri wa wizara ya maji , kilimo, ofisi ya Waziri mkuu Kilimo tena Ofisi ya rais mahusiano na uratibu na hatimae kilimo tena hadi sasa
Shughuli hizi chini ya Marais wa awamu zote nne umenipa uzoefu mkubwa wamasuala ya kitaifa na kuniwezesha kuifahamu vema Nchi yetu. Mimi nimiongoni mwa Watanzania wachache, wanaoijua Tanzania ya leo nakubashiri Tanzania ya kesho.
 
Kama mwanafunzi mzuri wa nafasi mbalibali, walioniundisha waliozingatia hazina ya uzoefu, naamini uzoefu niliopata utanisaidia sana katika uongozi wa nchi yetu iwapo chama changu kitanipendekeza na hatimayekuchaguliwa na watanzania kwa Rais wa nchi yetu

Pamojana yote hayo haitakuwa rahisi kwangu kufanya uamuzi wa kugombea nafasi ya urais.
 
 Hii ni kwa sababu natambua majukumu na wajibu wa Rais ulivyo mzito wa kuongoza watanzania karibu million hamsini (50)na zaidi kwa ulinzi wa matumaini na matamanio yao ya nyakati.

Hata hivyo, baada ya tafakuzi nimeridhika kuwa uamuzi wa kugombea nafasihii ya juu kabisa katika nchi yetu ni sahihi na ni wakati mwafaka nahali ya kisiasa ilivyo kwa sasa, najiona kuwa mtu sahihi , kwa kuwaninayo nia ya kuipeleka nchi yetu katika ngazi ya juu zaidi kisiasa,kiuchumu na kijamii.

SERAYA JUMLA ZA NCHI
Baadaya maelekezo hayo ya utangulizi, sasa nizungumzie mambo ya msingi nahazina yanayohusu uongozi wa nchi yetu.
 
Endapo nitateuliwa na chama changu na kupata ridhaa ya watanzania na hivyokuchaguliwa kuwa Rais wa Jamuhuri yaMuungano wa Tanzania nitaelekezanguvu zangu katika kusimamia yafuatayo;-

  1. Tanzania inabaki kuwa nchi imara yenye Umoja, Amani na Mshikamano.

  2. Taasisi nzito hususani mihimili mitatu ya dola ya kitaifa ( Serikali, Mahakama na Bunge) Zinaimaimarishwa na kuwezeshwa ili zitekeleze majukumu yake sahihi kwa mujibuwa katiba

  3. Utumishi wa umma utafanyiwa marekebisho ili utekeleze wajibu wake kwa uadlifu na waladi

  4. Kusimamia na kuhakikisha uchumi wa nchi unaendelea kukua kwa viwango vya juu zaidi ( kufikia tarakimu mbili) na utengenezaji wa nafasi za ajira unaoendana na matamanio ya wananchi
  5. Kuhakikisha raia wa Tanzania (wazawa) Wanawezeshwa ili washiriki kikamilifu katika kuendesha uchumi wa nchi yao.
CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI TANZANIA NA WATAZANZANIA
Haitoshikuifahamu Tanzania kama nchi na historia yake bila kuelewa changamotochangamoto zinazowakabili wananchi. Iwapo Chama change kitaniteuakupeperusha bendere ya CCM, na kupata ridhahaa, yako mambo manneambayo yatashughulikiwa na serikali ya awamu ya tano chini ya uongoziwangu. Mambo hayo ni;-
  1. Umasikini wa kipato
Pamoja na mafanikioya kukua kwa uchumi na ungezeko la huduma za kijamii yaliyopatikanakatika awamu ya nne, bado ipo changamoto kubwa ya umasikini.
 
Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa asilimia 28.2 ya watanzania ni masikini.Kwa mujibu wa takwimu hizo, wananchi wanaokabiliwa na umasikini huo,wengi wao wananishi vijijini na kujishughulisha na kilio, ufugaji nauvuvi. 
 
Uduni wa maisha ya vjijini unaotokana na hali hiyo yaumasikini ni chanzo pia cha umasikini wa mijini. Vijana wengiwanahama vijijini kwenda mijini na hivyo kuongeza kundi la umasikiniwa mijini.

LAZIMA TUWEKEZEKATIKA KILIMO
Njia pekee yakupambana na umasikini wa kipato hususani kwa wananchi wa vijijini ,ni lazima tuwekeze katika sekta ya kilimo, inayojumuisha kilimomazao, ufugaji na uvuvi. Serikali chini ya uongozi wangu, itatiliakipaumbele cha juu katika mapinduzi ya kiimo na uchumi wa vijijiniambao utaleta mabadiliko katia maisha ya watanzania walio wengi.

Kwa kuzingatia uwezekano mkubwa ambao Tanzania inao katika kilimo na idadi kubwa ya watu wanaoishi vijijini (70% - 75%) ambao wanaendesha maisha yaokutokana na kilimo na shughuli za kiuchumi wa vijijini, uendelezajiwake utapewa nafasi zaidi katika kuleta mabadiliko na kujenga uwezoambao baadae unaweza kuenezwa katika sekta nyingine. Mbinuzitakazotumika katika kuboresha kilimo ni pamoja na
  1. Matumizi ya sayansi ya kilimo (kiimo cha kisasa na cha kibiashara)
  2. Utafiti wa huduma za ugani
  3. Kuboresha miundombinu ya vijijni hususani barabara, umeme, na umwagiliaji.
  4. Upatikanaji wa mikopo katika kilimo ili kubadilisha zana, hususan kuachana na jembe a mkono hatua kwa hatua hatimaye kuweka jembe la mkono katika makumbusho ya Taifa.
  5. Kuongeza thamani ya mazao ya kilimo kwa kuhusisha kilimo na viwanda.
  6. Kuwapatia wakulima masoko ya uhakika kwa mazao yao.
MIFUGO
Maendeleo ya mifugoyatazingatiwa ili kufanya tasnia hiyo iongeze uzalishaji na kuwabiashara ya kuaminika, kwa kuwekeza mipenyo ya matumizi ya ardhi ilikuhakikisha uzalishaji zaidi na ongezeko la thamani ili kuimarishamaisha ya wafugaji, Serikali yangu itaweka kipaumbele katikakusimamia matumizi ya ardhi hususan kutatua migogoro ya wafugaji nawakulima kwa ufupi yafuatayo yatatiliwa mkazo;-
  1. Kupima ardhi kwa nia ya kuwapatiawafugaji malisho ya mifugo yao.
  2. Kujenga malambo / mabwawa ili kuwapatia wafugaji maji hususani katika maeneo ya mifugo yao.
  3. Kuwapatia vikundi vya wafugaji mikopo kwa kutumia hati ardhi kama dhamana.
UVUVI
Uvuvi una uwezekanomkubwa wa kukua kwa kuzingatia Pwani kubwa, maziwa na mito ambayoTanzania imejaliwa. Serikali itaweka dhamira ya kuleta mabadilikokatika sekta hii ili iwe biashara yenye tija katika kuongezauzalishji zaidi na kuongeza kipato ch wavuvi.

Mkazo utakuwa zaidikatika kuimarisha vitendea kazi, kupanua masoko na kuhamasishauongezaji wa thamani kwa mazao ya uvuvi.

HATUA ZAKUCHUKUA.
Kwaujumla hatua zifuatazo zitachukuliwa;
  1. Kuhamasisha kilimo cha ufugaji na uvuvi wa kisasa na kibiashara kwa
  1. Kutumia maarifa ya kisayansi
  2. Zana za kisasa (kuweka jembe la mkono katika makumbusho)
  3.  
  1. Mikopo na bajeti
Kuongeza uwekezajikwa njia ya
  1. Bajeti ya serikali ili kugharamia elimu ya wakulima, wafugaji na wavuvi
  2. Utafiti na uzalishaji wa mbegu za mifugo kilimo na mabwawa ya samaki
  3. Miundombinu ya umwagiliaji
  4.  
     
  1. Mikopo
Mikopo toka benki yaKilimo Na Benki ya Raslimali

AJIRA KWAVIJANA NA MAENDELEO YA VIWANDA

Sualala ukosefu wa ajira kwa vijana ni kubwa kwa mujibu wa takwimu katikawizara ya kazi, vijana milioni moja wanaingia katika soko la ajiranchini kila mwaka kati ya hao ni vijana 200,000 tu ndio wanaopatakazi. Huu ni uwiano mbaya sana ambao kama hatushughulikiwa unawezakusababisha matatizo ya kijamii na kisiasa

Serikalinitakayoendesha itaweka dhamira ya kukabili changamoto hii ya ajirakwa kutazama zaidi ya ajira rasmi ili kujumuisha kujiajiri naongezeko la tija katika uzalishaji ili jujipatia kipato stahiki.

Katika kipindi chamiaka mitano ijayo, zitaendelezwa kitihada za kupata ufumbuzi wakupunguza tatizo la ajira nchini. Kipaumbele kitakuwa katika kukuzana kuanzisha viwanda vilivyo na uwezo wa kuajiri watu wengi kama vilevya nguo(Pamba), Korosho, Ujenzi na vyenye kuzalisha bidhaazanazotuwa na watu wengi wa ndani na nje.

Katika kipindi chamiaka mitano, serikali itahakikisha sekta za uzalishaji mali , kamavile kilimo, ufugaji, uvuvi , viwanda vikubwa vikubwa na vidogo nahuduma za kiuchumi kama mishati , uchukuzi na ujenzi vinatekelezamipango yao katika kupunguza umaskini na kuzaliza ajira

Katika miaka yakaribuni vijana wameonyesha uwezo mkubwa wa kubuni ajira nakujiajiri, hatua ambazo zinastahili kupongeza kutiwa moyo na kuwezamfumo ya kuwawezesha.
 
 Ajira katika tasnia zilizokuwa kwa haraka nikatika masuala ya mitindo, miziki na filamu kama kina diamondplatinamz , Banana zoro na Binti yangu lady Jay dee, ommy Dimpoz,Christian Bella. 
 
Wabunifu wa mitindo kama vile Mustafa Hasani, AsiaIdarous, Filamu kama kina marehemu Stephen kanumba na Mtitu Gama.Leohii tasnia hizi zinaajiri mamlioni ya vijana.

Vijana mafundiwanatengeneza ajira katika Nyanja za ufundi, Viko viwanda visivyorasmi katika kila mji, kama uundaji bidhaa za vyuma, Ufundi bomba,Useremara, Ufundi umeme na umakenika wanatoa huduma kwa maelfu yawateja.
 
Katika jiji la DSM mfamo gerezani na Tabata dampo na hapaMwanza makoroboi. Vijana wanajiajiri katika teknolojia mpya hasaTEHAMA. Wanaunda mifumo ya kusisimua ya kumpyuta na hata simu zamkononi na kumuwezesha mtumiaji kutatua matatizo mbalimbali.

Vijana na mifumo yausafiri wa umma kwa kutumia baiskeli, pikipiki na pikipiki za miguumitatu zimeongeza ajira.
 
Wafanyabiasharamaarufu kama wamachinga, hawa huuza chochote unachohitaji, kuanziamagazeti na mahitaji mengine. 
 
Kundi hili linahitaji kuwekewa mipangokwa kutengewa maeneo ya biashara badala ya kukamatwa kamata kilakukicha. Mama ntilie ni kundi linalotoa huduma muhimu ya chakula hasamijini.
Source mpekuzi
 
TOA MAONI YAKO HAPA LAKINI MATUSI HAPANA .

Saturday 30 May 2015


Mabingwa mara 12 wa Kombe la FA, Arsenal baada ya ushindi wa jana dhidi ya Aston Villa.

Arsenal wakisherehekea ubingwa wao wa FA.

Theo Walcott akiifungia Arsenal bao la kwanza katika dakika ya 40.(P.T)

Walcott akishangilia bao hilo.

Alexis Sanchez (kushoto) akipiga shuti lililojaa wavuni na kuiandikia Arsenal bao la pili.

Per Mertesacker akipiga mpira wa kichwa uliozaa bao la tatu kwa Arsenal.

Olivier Giroud akifanya hitimisho kwa kutupia kambani bao la nne.
ARSENAL imetwaa Kombe la FA baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villa katika fainali iliyopigwa katika Uwanja wa Wembley usiku huu.
Mabao ya ushindi ya Arsenal yamefungwa na Theo Walcott dakika ya 40, Alexis Sanchez dakika ya 50, Per Mertesacker dakika ya 61 na Olivier Giroud aliyeingia kipindi cha pili na kufunga bao dakika ya 90.
Kwa matokeo ya jana, Arsenal wameweka rekodi ya kulichukua kombe hilo mara nyingi kuliko timu nyingine yoyote wakiwa wamelitwaa mara 12.

1_11381.jpg
1_3f5b8.jpg
1_43040.jpg
1_54897.jpg

 SOURCE MJENGWA

TUMA MAONI YAKO LAKINI MATUSI HAPANA


UTANGULIZI:

Ndugu zangu wana-CCM na Watanzania wenzangu,

Hii ni siku muhimu kwangu na kwa nchi yetu. Leo nimeamua kuwaita ili kuwatangazia rasmi Watanzania wenzangu azma yangu ya kutaka kuomba ridhaa ya chama chetu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), niweze kuteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nasema hii ni siku muhimu kwangu kwa sababu naamini historia yangu itainakili kama ni siku ambayo kwa mara ya pili katika maisha yangu nimejitokeza kuwania kuiongoza nchi yetu kupitia chama chetu. Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi hapa nchini nilipojitokeza nikiwa pamoja na Rais Jakaya Kikwete; wakati ule sote tulikuwa wanasiasa vijana. Tulikwenda pamoja kuchukua fomu ndani ya Chama na baadaye tukafanya mazungumzo ya pamoja na waandishi wa habari. Tulileta hamasa kubwa pale tulipofanya jambo ambalo halikuzoeleka kwa Watanzania kwa kutangaza kwamba yeyote atakayepita kati ya wawili sisi basi mwenzake ambaye hatafanikiwa angemuunga mkono.

Ningeweza kujitokeza tena mwaka 2005 lakini nikaamua kwa dhati kabisa kumuunga mkono moja kwa moja Rais Jakaya Kikwete.
 
 Nikiwa Mwenyekiti wa Kampeni niliwaongoza wenzangu kufanikisha ushindi mkubwa wa mgombea tuliyemuunga mkono na baadaye ushindi mkubwa wa asilimia 80 wa Chama Cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu wa 2005.

Nitaeleza kwa nini nimeamua kujitokeza tena mwaka huu na kwa nini naamini mimi ndiye mtu sahihi wa kuiongoza nchi yetu wakati huu. Mpaka hapa itoshe tu kuwaeleza ni kwa kwa nini naamini leo ni siku muhimu kwangu.

Lakini nasema ni siku muhimu kwa nchi yetu pia. Nasema hivyokwa sababu naamini inajibu wito wa mahitaji ya sasa ya uongozi wa Taifa letu wa kumpata kiongozi imara atakayewaongoza Watanzania kujenga taifa imara. Na hili pia nitalieleza kwa kina.

Hali  ya  Nchi  na  Matarajio  ya  Watu:
Miaka 48 iliyopita katika jiji hili la Arusha, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage alianzisha mchakato wa kujenga taifa huru kiuchumi na kupiga vita maadui umaskini, ujinga na maradhi kwakutumia silaha ya kujitegemea. 
 
Leo hii, wakati taifa likijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu ujao, hatuna budi kutafakari tulikotoka, tulipo na tunapotaka kwenda ili tuweze kubuni upya mikakati ya kuhitimisha azma aliyo kuwa nayo Mwalimu, ili tujenge taifa huru, lenye utulivu, mshikamano, amani na maendeleo.

Nchi yetu hivi sasa inapita katika kipindi kigumu cha mpito katika maeneo yote makuu ya maisha yetu – katika siasa, katika uchumi na katika maisha ya kijamii.

Kisiasa, tumeshuhudia kuongezeka kwa vuguvugu la mfumo wa vyama vingi ambapo ushindani kati ya vyama vya siasa unazidi kuwa mkali na kwa bahati mbaya kufikia sura ya kuonekana kama vile ni mapambano ya watu binafsi badala ya mapambano ya sera na dira ya kuongoza nchi. 
 
Tunashuhudia kuongezeka uhasama binafsi kati ya wanasiasa ndani ya chama kimoja kimoja na pia kati ya wanasiasa wa chama kimoja dhidi ya kingine. Kadiri siku zinavyokwenda, hali inazidi kuzorota na ikiachiwa kuendelea nchi yetu inaweza kujikuta mahali pabaya. 
 
Kukua kwa ushindani ni jambo jema linalokomaza na kurutubisha demokrasia yetu na tukiwa na ushindani wenye afya unaweza kuwa chachu ya kuleta mabadiliko mema kwa wananchi na kupelekea kuongezeka kwa kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi yetu. 
 
Kinyume chake ushindani unaochukua sura ya chuki binafsi au kukomoana na hata kulipizana visasi si ushindani wenye tija na tunapaswa kuutafutia tiba. 
 
Tunahitaji uongozi imara kusimamia kipindi cha mpito kutoka siasa muflisi za aina hii na kuelekea kwenye siasa mpya zinazoimarisha ushindani wenye tija unaojikita katika kushindana katika kuwapatia huduma bora Watanzania.

Kiuchumi, tumeshuhudia ukuaji mzuri na kuongezeka kwa mapato ya ndani ya Serikali na uimarishaji wa mfumo wa uwajibikaji na ulipaji kodi.
 
 Kwa upande mwengine, Serikali ya Rais BenjaminiMkapa na Rais Jakaya Kikwete imefanya kazi kubwa katika uendelezaji wa sekta ya mafuta na gesi asilia ambapo kiwango kikubwa cha gesi asilia kimegunduliwa.
 
 Tanzania sasa imekuwa ni miongoni mwa nchi zinazovutia uwekezaji mkubwa katika sekta hiyo ambayo inatajwa kwamba inaweza kuja kubadilisha kabisa maisha ya Watanzania. 
 
Hata hivyo, kipindi hiki cha mpito kuelekea ujenzi wa uchumi wa kisasa kimeshuhudia kuongezeka kwa hofu na wasiwasi miongoni mwa wananchi kwamba hawatonufaika naukuaji huu wa uchumi na ugunduzi wa utajiri mkubwa wa gesi asilia.
 
 Kwa upande mwingine, vijana wanataka kuona ukuaji wa uchumi na ugunduzi wa utajiri huo unakwenda sambamba na uzalishaji wa ajira zenye maana ili waweze kukabiliana na changamoto za maisha yao.
 
 Niliwahi kusema kwamba tatizo la ukosefu wa ajira likiachiwa bila ya kutafutiwa ufumbuzi imara ni bomu linalosubiri kulipuka. 
 
Vijana wasio na ajira hupoteza matumaini na ni rahisi kughilibiwa kuingiza nchi katika machafuko.Tunahitaji uongozi imara kuweza kuikabili hali hiyo na kuitafutia suluhisho maridhawa.

Kijamii, kipindi cha karibuni tumeshuhudia mabadiliko makubwa ya tabia miongoni mwa raia katika hali ambayo haijawahi kuwa sehemu ya utamaduni wa Watanzania.
 
 Kumekuwa na ongezeko la kutisha la matukio ya uhalifu linalokwenda sambamba na wananchi kuonyesha wanapoteza imani na taasisi zinazosimamia sheria na usalama na kuamua kujichukulia sheria mikononi mwao. 
 
Kumeripotiwa matukio mengi yakiwemo ya kuvamiwa vituo vya polisi, askari kupigwa na kuporwa silaha, matumizi makubwa ya nguvu katika utatuzi wa migogoro mbalimbali hasa ile ya kijamii, mathalani migogoro ya wakulima na wafugaji, mivutano ya kidini na pia mivutano baina ya viongozi wa dini wenyewe kwa wenyewe na baina ya viongozi wa dini na wale wa Serikali.
 
 Matokeo yakemshikamano wa taifa nao unaingia majaribuni. Mara nyingine wananchi wanatuuliza viongozi iwapo hii ndiyo nchi tuliyoachiwa na waasisi wetu. Tunahitaji uongozi imara wa kukabiliana na changamoto hizi na kurudisha mshikamano wa taifa letu na watu wake.


Watanzania  Wanataka  Mabadiliko;
Ndugu zangu, mnaweza kujiuliza kwa nini nimeyaeleza yote hayo na yana mahusiano gani na dhamira yangu ya kutangaza nia ya kutaka kuiongoza nchi yetu kupitia CCM?

Nimeyaeleza haya kwa sababu haya na matukio mengine yanayoendelea nchini yamepelekea Watanzania kutaka mabadiliko. 
 
Watanzania wanataka mabadiliko yatakayowawezesha kuzishinda changamoto hizi na kuwaongoza kujenga Taifa imara ambalo kila mwananchi wake anaishi akiwa na uhakika wa mahitaji yake muhimu na papo hapo akijiridhisha kwamba leo yake ni bora kuliko jana yake, na kesho yake itakuwa bora zaidi kuliko leo yake.
 
 Kwa maneno mengine, Watanzania wanahitaji mabadiliko yatakayowapa uongozi imara unaoweza kuwaongoza kujenga taifaimara. Hii ndio Safari ya Matumaini.

Chama chetu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), na watangulizi wake, TANU na ASP, kimepata bahati ya kuungwa mkono na Watanzania tokea enzi za kupigania uhuru, wakati wa Uhuru wa Tanganyika na Mapinduzi ya Zanzibar, na pia miaka yote tokea Uhuru, Mapinduzi na hatimaye Muungano wetu. Watanzania hawajawahi kushuhudia chama kingine kikiongoza Serikali zetu zaidi ya CCM. Wamekiamini na wanaendelea kukiamini.
 
 Hata katika yale majimbo machache ya nchi yetu ambayo hatukufanya vizuri katika uchaguzi, ukiangalia kwa undani utaona si kwamba watu wa maeneo hayo wana matatizo na CCM kama Chama bali wana matatizo na baadhi ya viongozi ambao walishindwa kukiwakilisha vyema Chama na kutambua matakwa ya wananchi hao.

Mimi naamini kwamba hata katika kipindi hiki ambapo Watanzania wanaonekana kutaka mabadiliko bado wanaendelea kuamini kwamba watayapata mabadiliko hayo ndani ya CCM. 
 
Lakini kama alivyotupa wasia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 1995 wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi hapa nchini, Watanzania wasipoyapata mabadiliko hayo ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM. 
 
Mimi naamini kwamba CCM tunao uwezo wa kuwapa Watanzania mabadiliko wanayoyataka. Tuwape imani na imani hiyo iwe ni ya dhati na ya ukweli kwamba CCM inao uwezo wa kuwapa uongozi imara wanaouhitaji kwa ajili ya kujenga taifa imara.

Vyama vya siasa vinajumuisha watu na vinaongozwa na watu. Moja ya hulka ya binadamu ni kubadilika kulingana na mahitaji ya mazingira anayoishi.
 
 Kwa maneno mengine, binadamu ni ‘dynamic’. Kwa sababu hiyo basi, hata vyama vya siasa vinapaswa kuwa ‘dynamic’.
 
 CCM haijapata kuwa na upungufu wa sifa ya ‘dynamism’. Kwa zaidi ya miongo mitano sasa, CCM (na kabla yake TANU na ASP) iliweza kubadili dira na mwelekeo wake ili kwenda sambamba na mahitaji ya Watanzania ya wakati husika. 
 
Ndiyo maana tumepita katika vipindi tofauti vya mpito kwa mafanikio makubwa licha ya changamoto nyingi zilizotukabili. 
 
Tanzania imeendelea kuwa nchi ya amani licha ya kubadili mfumo wetu wa siasa kutoka ule wa chama kimoja kuja vyama vingi; licha ya kubadili mwelekeo wa uchumi wetu kutoka ule wa dola kumiliki njia zote kuu za uchumi kuja katika uchumi wa soko unaozingatia ushiriki mpana wa Watanzania wa matabaka yote; na hata karibuni kabisa katika mchakato wa kuipatia nchi yetu Katiba mpya.
 
Tanzania tumeweza kufanya mabadiliko ya uongozi mara nne katika hali ya amani na maelewano, jambo ambalo nchi nyingi za Afrika zimeshindwa.
 
 Ni imani yangu kwamba tukijikubalisha tunaweza tena kuwapa Watanzania wanachokitaka katika zama hizi za sasa.
 
 Lakini ni lazima tuoneshe dhamira hiyo kwa dhati ili, kama alivyotuasa Mwalimu Nyerere, Watanzania wasiyatafute mabadiliko hayo nje ya CCM. 
 
Nasisitiza tena kwamba CCM inao uwezo wa kuwapa Watanzania mabadiliko wanayoyataka, lakini pia wananchi wana hiali kuchagua mabadiliko wanayoyataka.

Uongozi  unaohitajika  kuleta  mabadiliko  yanayotakiwa:
Rais Jakaya Kikwete amefanya kazi kubwa katika kipindi chake na kama ambavyo amekuwa akisisitiza mara kwa mara katika hotuba zake za karibuni ni kwamba yeye ametekeleza wajibu wake kwa kuweka misingi imara ya ujenzi wa Taifa la kisasa lenye uchumi madhubuti na unaoweza kukua kwa kasi.
 
 Amesema anamwachia atakayemkabidhi uongozi wa nchi yetu baada ya yeye kumaliza muda wake kuendeleza pale atakapoachia.

Kwa maoni yangu ili kuifanya kazi hiyo na kuzikabili changamoto nilizozieleza, nchi yetu inahitaji uongozi wenye sifa zifuatazo:

-  Uongozi wenye uthubutu, usioogopa kufanya kufanya maamuzi magumu;
-    Uongozi thabiti na usioyumba;
-    Uongozi makini na mahiri;
-    Uongozi wenye ubunifu na wenye upeo mkubwa;
-   Uongozi utakaozikabili changamoto kifua mbele na siyo kuzikimbia;
-    Uongozi unaoamini katika mfumo shirikishi katika ujenzi wa Taifa;
-    Uongozi unaozingatia muda katika kutekeleza majukumu yake.

Naamini pia kwamba wananchi wanataka Rais ajaye wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awe na sifa kuu zifuatazo:

-    Aweze kuwaunganisha Watanzania (kukabiliana na viashiria vya migawanyiko ya aina mbali mbali inayoinyemelea Tanzania);

-    Aweze kuja na sera na mikakati ya kuinua uchumi wa Tanzania na kukuza pato la Mtanzania;ikiwemo kupunguza tofauti ya kipato kati ya aliyekuwanacho na wasiokuwanacho;

-     Aweze kuja na sera na mikakati ya kuzalisha ajira kwa vijana wetu;

-     Aweze kutokomeza mianya ya rushwa kwa vitendo;
-    Aweze kuwa mfano wa kuchapa kazi na kuwajibika;
-     Asimamie nidhamu ya matumizi ndani ya Serikali;
-     Aweze kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali;
-     Aweze kutumia fursa yetu ya kijiografia kibiashara

Uongozi  Imara,Taifa  Imara
Naamini kwamba uongozi wa juu wa nchi katika nafasi ya Urais si kazi ya lelemama na unahitaji utashi. Kabla hata ya kutakiwa na wenzako ni lazima kwanza wewe mwenyewe uamini na uwaaminishe wenzio kwamba unao uwezo wa kuwaongoza wananchi wenzako. Na katika hilo, rekodi yako ni lazima izungumze na kulithibitisha hilo.

Binafsi nina hazina ya uzoefu na rekodi njema ya matokeo ya kazi nilizozifanya katika uongozi na utumishi wa umma ndani ya CCM na ndani ya Serikali. Nilianza kazi nikiwa Katibu Msaidizi wa CCM katika mikoa ya Shinyanga, Arusha na Moshi.
 
 Nimekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu ya CCM. Niliingia Bungeni mwaka 1985 na baadae mzee wangu, Rais Ali Hassan Mwinyi, akaniamini kwa kuniteua kuwa Waziri. 
 
Nimekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Ardhi, Makaazi na Maendeleo ya Miji, Waziri wa Mazingira, Waziri wa Maji na hatimaye Waziri Mkuu.

Miongoni mwa mafanikio ninayojivunia katika uongozi na utumishi wangu, na ambayo Watanzania wanayatambua na naamini wanayathamini, ni pamoja na:

-    Nikiwa Waziri wa Maji chini ya uongozi mahiri wa Rais Mkapa,tulithubutu kushawishi na kuongoza hatua za kukataa kufungika na makubaliano yaliyowekwa na wakoloni ambayo yalikuwa yanazizuia nchi zilizopakana na Ziwa Victoria zisiweze kufaidika ipasavyo na maji ya Ziwa hilo. Leo hii ndugu zangu wa Kanda ya Ziwa wanafaidika na ujasiri wetu katika kukabiliana na suala hilo zito.

-    Nikiwa Waziri wa Mazingira, tulipanda miti mingi zaidi kuliko wakati mwingine wowote tokea Uhuru na pia kuwakabili kikamilifu na kuwachukulia hatua waliochafua na kuharibu mazingira.

-    Nikiwa Waziri Mkuu, tulisimamia agizo la Rais Kikwete na kufanikisha utekelezaji wake ndani ya miaka miwili kwa kujenga shule nyingi za sekondari kuliko wakati mwingine wowote tokea Uhuru.

-    Kipindi hicho hicho, tulisimamia agizo la Rais Kikwete la kuanzisha Chuo Kikuu cha Dodoma na kuhakikisha kinakamilishwa kwa wakati. Leo hii Chuo Kikuu hicho ni fahari ya Tanzania.

Tunapomtafuta Rais wa Jamhuri ya Muungano ni lazima tukumbuke kwamba tunamtafuta mtu ambaye atakuwa pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika nchi yetu. Na kwa Chama Cha Mapinduzi tunamtafuta mtu ambaye atakuwa pia Mwenyekiti wa Chama chetu.

Naamini kwa vigezo vyote, nina kila sifa ya kubeba dhamana hizo nzito. Katika mambo ambayo najivunia na sitoyasahau katika historia yangu ni kushiriki kwangu kuilinda nchi yangu pale ilipohitajika. 
 
Nilishiriki kikamilifu katika Vita vya Kagera nikiwa miongoni askari wa mstari wa mbele wa mapambano. Nikiwa Mbunge nilipata heshima ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama. Naamini Watanzania hawatakuwa na wasiwasi wa usalama wao nikiwa Amiri Jeshi Mkuu.

Nimeeleza uzoefu wangu kwenye Chama na huo hauhitaji maelezo zaidi. Ninakijua vyema Chama Cha Mapinduzi kiasi cha kutosha kabisa kukiongoza kama Mwenyekiti wake pale wakati utakapofika.
 
 Wana-CCM wanajua nikikabidhiwa uongozi, Chama chetu kitakuwa chini ya nahodha madhubuti, mzoefu na asiyeyumba.

Kutokana na rekodi yangu hii, naamini ninazo sifa za kuwaongoza Watanzania wenzangu katika zama mpya za ujenzi wa Taifa la kisasa lenye watu wazalendo walioshikamana na lenye uchumi imara unaomnufaisha kila Mtanzania. Naamini ninao uwezo wa kuwapa Watanzania Uongozi imara kwa ajili ya ujenzi wa Taifa Imara.

Dira  yangu  na  Matarajio  ya  Watanzania
Mfumo tuliojiwekea hapa nchini unaelekeza kila chama cha siasa kinachosimamisha mgombea Urais na kinachowania kuongoza nchi yetu kuja na Ilani ya Uchaguzi ambayo ndiyo inayoweka misingi ya sera zitakazofuatwa na Serikali itakayoongozwa na chama hicho pale kinapopewa ridhaa ya kuongoza nchi.
 
 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa ni cha kupigiwa mfano katika kutayarisha Ilani bora na ndiyo maana mara zote kimepewa ridhaa ya kuongoza nchi yetu. Tumefanya hivyo tokea enzi za mfumo wa chama kimoja na tumeendelea kufanya vizuri katika mfumo wa kushindanisha sera kupitia vyama vingi. 
 
Najua kwamba Ilani ya CCM ya mwaka 2015 imo katika hatua za mwisho za kukamilishwa na itakapopata baraka za vikao vya Chama itakuwa ndiyo msingi wa utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano itakayochaguliwa Oktoba mwaka huu. 
 
Hata hivyo, naamini pia kwamba mgombea mwenyewe anayetaka ridhaa ya Chama na ya Watanzania kuongoza nchi naye anapaswa kueleza dira yake.

Mimi, baada ya kutafakari kwa kina changamoto tulizo nazo na matarajio na matumaini waliyo nayo Watanzania, naamini kwamba Uongozi imara unaolenga kujenga Taifa imara unapaswa kuwa na dira yenye malengo yafuatayo:

-    Kuimarisha Muungano wetu kwa kuyashughulikia yanayotutenganisha na kuyafanyia kazi ili yasivuruge yale yanayotuunganisha ambayo ni mengi zaidi na makubwa zaidi.

-    Kushughulikia matumizi mabaya ya siasa za udini na ukabila kwa kuimarisha siasa zilizoshiba uzalendo na zenye kutuelekeza kwenye Utanzania wetu.

-    Kujenga uchumi imara na wa kisasa, na ambao ni shirikishi unaomnufaisha kila Mtanzania aliyeko mjini au kijijini. Tunapaswa kubadili hali tuliyo nayo sasa ambapo Kilimo kinaonekana kama kimesahauliwa na wakulima wetu wanaonekana wanakata tamaa.
 
Wafugaji na wavuvi nao wanahisi sekta zao hazijapewa umuhimu unaostahiki. Tunahitaji kuondokana na hali iliyopo sasa ya kuwa Taifa linalouza malighafi na badala yake kuwa Taifa linalosindika na kusarifu mazao na kutengeneza wenyewe bidhaa zitokanazo na malighafi yake. 
 
Ndani ya miaka mitano ijayo tutahakikishatunaiondolea Tanzania sifa ya kusafirisha malighafi na badala yake kusindika mazao yanayozalishwa hapa nchini kama pamba, kahawa, chai na korosho na kuyaongezea thamani (value addition).Mkakati huu utazalisha ajira nyingi na kuongeza mapato ya fedha za kigeni nchini.
 
 Tunahitaji kujielekeza kwenye kujenga viwanda na kuleta ajira. Tuna vivutio vingi sana vya utalii lakini bado Tanzania inapitwa na nchi kama Afrika Kusini katika kuingiza idadi kubwa ya watalii.
 
 Kwa nini nchi kama Dubai iweze kuvutia watalii kwa mamilioni na Tanzania tushindwe? Tunapaswa kukabiliana kikamilifu na hisia zilizopo miongoni mwa wananchi kwamba Tanzania hainufaiki ipasavyo na utajiri wa rasilimali zake nyingi ilizo nazo. 
 
Tutajipanga zaidi kuhakikisha tunanufaika kama nchi na rasilimali zetu kama madini na gesi asilia. Hii ndio Safari ya Matumaini

-    Kukuza kipato cha wananchi na kunyanyua hali za maisha ya watu wetu. Tunapaswa kuhakikisha kuwa ukuaji wa uchumi tunaouzungumzia unamnufaisha Mtanzania aliyeko mjini au kijijini na kwamba hali za Watanzania wa matabaka yote zinanyanyuka na kwamba wanaridhika na kuuona uhalisi wa ukuaji wa maendeleo tunayoyazungumzia.

-    Kuondokana na sifa mbaya ya kuwa Taifa ombaomba. Kwa wingi wa rasilimali tulizo nazo na neema ya ardhi, maziwa, mito na bahari Tanzania tuna kila sababu ya kuacha kuwa ‘bakuli la ombaomba’ na badala yake kuwa ‘mkoba wa neema’ katika Afrika.We can transform our nation from being the begging bowl to become the bread basket of Africa.

- Kujenga mfumo mpya wa elimu unaojielekeza kuwatayarisha vijana wetu waweze kuajirika, kujiajiri na kushindana katika soko la ajira. 
 
Tumepiga hatua kadhaa katika elimu lakini kiwango cha elimu bado ni hafifu. Pamoja na kuwa na shahada (degrees), bado wahitimu wetu hawawezi kushindana kwenye soko la ajira. 
 
Wakati tunazungumzia kuunganisha soko la ajira katika Afrika Mashariki,hatuna budi kujikita kubadili mfumo wetu wa elimu na kuuelekeza kwenye mafunzo ya ufundi na stadi yanayowajenga wahitimu wetu kuwa wabunifu na wenye kujiamini katika kukabiliana na changamoto za maendeleo duniani.

-    Kuhakikisha tunakabiliana ipasavyo na kulipunguza kwa kiasi kikubwa kama si kulimaliza kabisa tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama. Ni jambo la kusikitisha kwamba tumezungukwa na mito na maziwa lakini bado watu wetu hawana maji ya kunywa hata ndani ya Dar es Salaam.

-    Kujenga na kusimamia mfumo imara wa kutekeleza sera na sheria tunazozitunga na kuzipitisha kwa lengo la kumtumikia Mtanzania na kumjengea uwezo wa kubadili maisha yake ili tuweze kwenda sambamba na viwango vya kimataifa. Tanzania imepata sera na sheria nzuri sana lakini utekelezaji wake umekuwa hafifu. 
 
Tumekuwa wepesi wa kutunga sera na sheria lakini wazito mno wa kuzitekeleza na kuzisimamia. Uongozi imara wenye kulenga ujenzi wa Taifa imara utahakikisha tunakuwa mfano wa utekelezaji wa sera na sheria tulizo nazo na mpya zitakazotungwa kukabiliana na malengo tuliyojiwekea.

Mambo haya niliyoyaeleza hapa ndiyo yatakayokuwa msingi mkuu wa utendaji wa Serikali nitakayoiongoza pale nitakapopewa ridhaa ya kubeba bendera ya CCM katika nafasi ya Urais na pia nitakapopewa ridhaa ya kuliongoza Taifa letu kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Ramani  ya  Uongozi  Imara  Ninaouamini 9 Leadership Roadmap)
Kama nilivyotangulia kusema, kazi ya kuongoza nchi si lelemama na hasa unapoongozwa na dhamira ya dhati na msukumo wa ndani ya nafsi unaojielekeza kubadilisha maisha ya wananchi wenzako waliokuamini uwaongoze. Kwa vyovyote vile, hiyo haiwezi kuwa kazi ya mtu mmoja. Ni kazi ya pamoja.
 
 Lakini ili muweze kufanya kazi kama timu moja iliyojipanga kisawasawa kuleta mabadiliko yanayohitajika na ili muweze kweli kutoa Uongozi imara unaojikita kujenga Taifa imara hapana budi kiongozi mkuu anayeongoza timu hiyo aweke ramani anayokusudia kuifuata katika kutoa uongoziimara anaoukusudia yaani ‘Leadership Roadmap’.

Pamoja na kuwa sehemu ya uongozi huko nyuma, kutakuwa na maamuzi na matumaini mapya. Ramani ya uongozi imaraninayokusudia kuutoa kwa wenzangu na ambayo nitaitumia kuiongoza timu yangu katika kuwatumikia Watanzania wenzangu itajikita katika maeneo yafuatayo:

1. Kurejea kwenye Katiba katika kuainisha nia, dhamira na malengo yetu ya kujenga jamii inayozingatia misingi ya demokrasia, udugu na amani. Muhimu katika hili ni kukemea tabia mbaya zinazochochea mfarakano katika jamii kama vile matumizi mabaya ya siasa za udini na ukabila.
 
Aidha moja ya misingi muhimu ya Katiba ni Muungano wetu. Itakuwa dhamira yangu kuimarisha misingi ya Muungano pamoja na udugu wa damu nahistoria ya ushirikiano iliyojengwa na waasisi wetu, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Amri Abeid Karume na kuyaenzi Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

2. Kujenga fikra mpya za kurejesha kujiamini na kufufua azma ya kujitegemea kama Taifa. Ni dhahiri kuwa pamoja na rasilimali zetu, bado Tanzania ni taifa tegemezi. Bado tunajidanganya kuwa wafadhili watatujengea nchi. Tukumbuke, nchi zinajengwa nawananchi wake. 
 
Nasi pia lazima tujikomboe kifkra na tuondokane na utamaduni wa kuwa tegemezi. Tuanze kwa kujipiga kifua kwa kujiamini kuwa tunaweza kujitegemea na kuijenga Tanzania sisi wenyewe.Kujiamini na kujitegemea ndio uhuru wa kweli.

3. Kujenga uzalendo, uadilifu ikiwa ni pamoja na kuimarisha uwazi katika shughuli zote za serikali na kupambana na rushwa.Watanzania tumepoteza uzalendo kwa kiasi kikubwa. Kuna vitendo vinavyoashiria kuwa hatuipendi tena nchi yetu. 
 
Tunashabikia wizi na rushwa. Inabidi turejee kwenye misingi ya taifa letu misingi ya uadilifu na uzalendo. Tukumbuke kuwa hatuwezi kujenga uchumi wa kisasa kama tutaruhusu rushwa ishamiri.
 
 Wawekezaji hawataleta mitaji yao kwa wingi kama rushwa itaendelea kutawala katika huduma serikali na wananchi hawawezi kupata huduma bora kama rushwa itaendelea kutawala. Ni lazima tuipinge rushwa kwa vitendo sio maneno.

4. Kujenga Serikali madhubuti, makini na yenye nidhamu inayoendeshwa kwa misingi ya sheria, uwazi na uwajibikaji.Maendeleo ya watu hayawezekani bila serikali kusimamiautekelezaji sera na miradi na kuleta ufanisi katika kutoa huduma na kusimamia maendeleo. Tumekuwa wepesi wa kutunga sera lakini wazito wa kuzitekeleza na kuzisimamia.


5. Kuleta msukumo mpya wa ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi katika ujenzi wa uchumi wa kisasa na unaojitegemea. Sekta binafsi ndiyo nyenzo ya uchumi imara. Inazalisha mali, ajira na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa kwa kulipa kodi.
 
 Ilisekta hii itoe mchango unaotakiwa katika maendeleo ni lazima ifanye kazi na serikali kwa karibu. Tukumbuke, bila uchumi imarahakuna huduma bora!


6. Uwekezaji katika huduma za jamii. Elimu na afya bora, mazingira, makazi safi na maji salama ndiyo mihimili ya maendeleo ya watu.
 
 Hii inawezekana tu iwapo serikali itakuwa na sera na utashi wa kuutambua uboreshaji wa huduma za jamii kama ndiyo lengo kuu la maendeleo ya nchi. Serikali nitayoiongoza itahakikisha kuwa kila Mtanzania anapata elimu bora na inayogharamiwa na serikali kama mimi na wenzangu tulivyopata. 
 
Wakatitunazungumzia kuunganisha soko la ajira katika Afrika Mashariki, hatuna budi kurekebisha mfumo wetu wa elimu na kuuelekeza kwenye mafunzo ya ufundi na ustadi yanayowajenga wahitimu wetu kuwa wabunifu, wenye kujiamini, wenye uwezo kushindana katika soko la ajira na wa kujiajiri. Napenda kusisitiza kuwa elimu ndiyo muhimili wa maendeleo, ndiyo mkombozi wa kweli wa binadamu. Mimi ni mfano hai wa ukombozi wa elimu. 
 
Elimu ndiyoimenivusha kutoka kijijini kwetu Ngarash na kunipa upeo wa kitaifa. Mama akiwa na elimu atajua umuhimu wa kumpeleka mwanae shule, anapata lishe bora na chanjo stahili na kuwa anaishi katika mazingira safi. Elimu ndilo jibu la umaskini, maradhi na ujinga.Taifa lililo elimika ni taifa lenye maendeleo.
 
7. Kujenga uchumi shirikishi unaolenga kuondoa umaskini.Mkakati wa kuondoa umaskini Tanzania lazima ujikite kwenye nguzo za ushiriki wa kila Mtanzania katika uchumi wa taifa. 
 
Kwa misingi hii, tukiweza kupunguza umaskini, tutaweza pia kupunguzatofauti za kipato ambazo tukiziacha ziendelee kukua kwa kiasi cha sasa, zinaweza kuhatarisha utulivu na amani katika jamii yetu.Uchumi shirikishi ndio silaha dhidi ya umaskini.

8. Kuimarisha ulinzi wa nchi na usalama wa raia na ujirani mwema.Itakuwa nia yangu kuimarisha misingi iliyojengwa kulinda na kudumisha umoja na amani nchini. 
 
Kadhalika, nitahakikisha kuwa usalama wa mipaka ya Tanzania unaimarishwa kwa misingi ya ujirani mwema na kutanzua migogoro na matatatizo yoyote na nchi jirani, kwa njia ya diplomasia na mazungumzo.

Hitimisho:
Hii ndiyo misingi na dira ya uongozi wangu. Nachelea kusema kuwa haitakuwa kazi rahisi. Lakini kwa ushirikiano wa kila mmoja na maamuzi magumu, yote yanawezekana.
 
 Tumeona nchi nyingi zilizosimamiwa na utawala thabiti wa serikali za kimaendeleo zikikabili na kupunguza umaskini katika kizazi kimoja. Kama mataifa mengine yamefanikiwa, tena bila raslimali kama zetu, kwa nini sisi tushindwe? 
 
Tuna kila sababu ya kufanya maamuzi magumu sasa ili kuwajengea Watanzania matumaini mapya ya maendeleo. Naomba nisisitize kuwa katika uongozi wangu hakutakuwa na nafasi ya majungu, na visasi. Hatutaangalia nyuma bali tutasonga mbele kwani ndicho Watanzania wanakitarajiakutoka kwa uongozi uliojengwa kwenye misingi bora.

Ndugu Watanzania:-
Ni maono yangu kuwa siku si nyingi nchi yetu itaanza safari yenye uelekeo wa matumaini na neema tele kwa wananchi.

Ni maono yangu kuwa siku si nyingi sisi kama Watanzania kwa umoja wetu tutajivunia kuishi katika nchi tunayoipenda na inayoendeshwa kwa misingi ya utawala bora, chini ya serikali ya kimaendeleo iliyojengwa kwenye fikra mpya za uzalendo, uadilifu, utendaji na uwajibikaji.

Ni maono yangu kuwa Peke yangu sitaweza, lakini kwa maamuzi magumu na ushirikiano wa kila mmoja wetu ikiwa ni pamoja na wagombea wenzangu ndani ya CCM, inawezekana kuanza safari hii ya Matumaini Mapya.

Kabla ya kumaliza hotuba yangu hii fupi, kuna mambo matatu ningependa kuyaweka wazi hapa.

La kwanza, linahusu msingi wa uongozi ninaouamini na ambao nimeusema mara kadhaa hapa. Msingi huo ni UWAJIBIKAJI.Watanzania wananifahamu mimi si mtu wa maneno, ni mtu wa vitendo. Naamini kwa dhati kabisa kwamba huwezi kuwa na Uongozi imara utakaoweza kusimamia ujenzi wa Taifa imara iwapo huna ujasiri wa kuwajibika. Mimi nimeongoza kwa mfano, na pale ilipobidi, nilikubali kuwajibika na kubeba dhamana ya uongozinilipojiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu.

La pili, mimi si mtu wa visasi. Siamini katika kuangalia ya nyuma. Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Na kwa nini tuangalie nyuma wakati kama taifa tuna kazi kubwa sana mbele yetu inayohitaji kufanywa? Mimi ni Mkristo; najifunza kutoka kwa Bwana Yesu ambaye alipoulizwa: “Nisamehe mara ngapi?” Alijibu, “Samehe mara sabini mara saba”. Nitaenzi na kudumisha utamaduni huu wenye sura ya utu na heshima.

La Tatu, natambua kwamba dhamana ya Urais ni shughuli nzito hasa kwa taifa ambalo lina changamoto nyingi. Nataka niwahakikishie Watanzania wenzangu kwamba afya yangu ni njema kuweza kuwatumikia katika jukumu hili zito. Pamoja na vijineno vinavyosemwa pembeni, mimi mwenyewe ndiye ninayejijua zaidi. Nawahakikishia kuwa nisingekuja hapa leo na kueleza nia yangu hii ingekuwa sina uhakika na afya yangu.

Natoa RAI kwa Chama changu cha CCM, nadhani umefika wakati kwamba tutende tofauti na mazoea, watu wote walionyesha nia ya kutaka kuongoza, liundwe jopo la madaktari wa ndani na nje ya nchi tupimwe afya zetu, kwa hili najitolea kuwa wa KWANZA KUPIMWA afya yangu

Safari tuianze leo, hatuna kesho nyingine.
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza
       Source Mpekuzi blog