Tuesday, 2 June 2015
22:33
Unknown
Vumbi la kinyang’anyiro cha uteuzi wa kuwania urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), linaanza rasmi Dodoma leo kwa wanachama wake watano kuchukua fomu wakiomba uteuzi huo.
CCM imepanga kuanzia leo Juni 3 hadi Julai 2, mwaka huu, kuwa siku za
kuchukua na kurudisha fomu za wanachama wake wanaoomba uteuzi kuwania
urais.
Uteuzi huo ni kwa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini
kwa uteuzi wa Rais wa Zanzibar, fomu zitakuwa zikitolewa kisiwani
Unguja.
Tayari wanachama wa CCM kadhaa wamekwisha kutangaza nia ya kumrithi
Rais Jakaya Kikwete huku wengine zaidi wakitarajiwa kufanya hivyo.
Kwa mujibu wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) wa
Oganaizesheni, Dk Muhammed Seif Khatib, uchukuaji wa fomu hizo unaanza
rasmi leo.
Khatib aliwaambia waandishi wa habari jana katika Makao Makuu ya CCM
‘White House’, Mtaa wa Nyerere mjini Dodoma kuwa fomu zitaanza kutolewa
saa nne asubuhi.
Alisema kwa mujibu wa orodha waliyonayo, wanachama watano watachukua
fomu hizo kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 10:30 jioni, na kila mmoja
amepewa saa moja na wametenga muda wa kuzungumza na waandishi wa habari
kwa wagombea ambao wataona inafaa kwao.
“Uchukuaji huu wa fomu haukufuata umaarufu wa mtu, ujuzi, alfabeti,
nafasi yake katika Chama na Serikali, bali umefuata aliyewahi kutoa
taarifa kwa Chama,” alisema Khatib akifafanua uchukuaji huo.
Alimtaja wa kwanza kuchukua fomu kuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya kuanzia saa 4 kamili hadi
saa 5:30.
Profesa Mwandosya atafuatiwa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Stephen Wassira kuanzia saa 5:30 na atafuata Waziri Mkuu wa zamani,
Edward Lowassa atachukua fomu kuanzia saa saba kamili.
Wa nne atakuwa Waziri wa zamani wa Muungano, Balozi Amina Salum Ali
kuanzia saa 8:30 mchana na pazia la ufunguzi litafungwa saa 9:30 alasiri
na mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Charles Makongoro Nyerere.
Mbali ya wanachama hao watano, wanaCCM wengine ambao wametangaza nia
ya kuwania urais ni Lazaro Nyalandu, Frederick Sumaye, Profesa Sospeter
Muhongo, January Makamba, Mwigulu Nchemba na Luhaga Mpina.
Wanaotajwa ni pamoja Bernard Membe, William Ngeleja, Dk Titus Kamani,
Luhaga Mpina, Mizengo Pinda, Dk Asha-Rose Migiro, Shamsi Vuai Nahodha,
Dk Emmanuel Nchimbi na Dk Hamis Kigwangalla.
Katibu huyo wa Oganaizesheni alisema uchukuaji huo wa fomu
utazingatia taratibu zilizowekwa na CCM na kutakuwa na fomu tatu
zitakazopewa wagombea.
“Fomu ya kwanza itahusu maelezo binafsi ya mgombea, itahusu uzoefu na
ujuzi wake, nyingine itakuwa ya kujaza orodha ya wadhamini wake na
nyingine ya masharti kama yalivyokubaliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa,”
alifafanua Dk Khatib.
Alisema katika wadhamini, mgombea atatakiwa kupata wadhamini 450
kutoka katika mikoa 15 ya Tanzania Bara na mikoa mingine mitatu ya
Tanzania Zanzibar.
“Mjumbe yeyote wa Mkutano Mkuu wa Taifa haruhusiwi kumdhamini
mgombea, pia mwanachama haruhusiwi kudhamini mgombea zaidi ya mmoja,”
alifafanua.
Alisema ili kuonesha uhalali wa fomu hizo za wadhamini, zitapaswa
kuwa na mhuri wa Katibu wa CCM wa wilaya husika pamoja na saini yake na
pia mdhamini atapaswa kusaini na kuandika kadi yake ya uanachama.
Alisema wagombea hao watakapofika kuchukua fomu, wanapaswa kuwa na
ada ya Sh milioni moja na watasaini daftari maalumu kuonesha ndio
waliochukua fomu.
“Tumepanga muda wa saa moja moja na nusu kwa kila mgombea kuwapo
hapa. Na akishachukua fomu tumepanga anayetaka azungumze na waandishi wa
habari kwenye Ukumbi wa NEC,” alisema Dk Khatib.
Alisema katika chumba cha uchukuaji wa fomu, wataruhusiwa mgombea
kuingia na watu wasiozidi 10.
“Katika chumba hiki (cha mikutano na
waandishi katika Makao Makuu) tutaruhusu mgombea kuingia na watu
wasiozidi 10… mkewe na jamaa zake wengine, wanaomsindikiza, sijui
wengine mnawaita wapambe, mimi nawaita wanaomsindikiza,” alisema Katibu
huyo.
Aliwataka wagombea wengine wanaotaka kuchukua fomu hizo kuwasiliana
mapema na ofisi yao kwani alisema wangependa kazi ya uchukuaji fomu
kudumu kwa siku zisizozidi tano ili shughuli nyingine ziendelee.
Sunday, 31 May 2015
22:30
Unknown
NAIBU
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, amesema
kwa sasa nchi ipo njia panda, hivyo kuna haja ya kutumia busara ili
kuchagua kiongozi atakayeleta maendeleo.
Kauli
hiyo aliitoa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki , wakati akizungumza na
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Tawi la Mwenge, kuhusu utandawazi na
maendeleo ya jamii.
January,
Mbunge wa Bumbuli, ambaye pia ametangaza kutaka kugombea urais, alisema
Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu ni muhimu kuliko zote,
kutokana na wananchi kuwa njia panda ambayo moja ina mashimo na nyingine
ina mafanikio.
Alisema
matamko mbalimbali ya viongozi wa dini katika sherehe za sikukuu na
mwaka mpya yanaonyesha nchi ipo njia panda kutokana na wananchi kukosa
amani ya moyo.
“Uchaguzi
huu una majaribu mengi, kuna viongozi wanafanya kazi ya kutoleana lugha
kali na kushutumiana wizi, tafadhali angalieni uchaguzi huu ni muhimu
na tunaweza tukachagua watu watakatuingiza shimoni ama watakaoweza
kutupeleka katika mafanikio,” alisema January.
Alisema
hiki ni kipindi cha tatu ambacho Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaingia
katika uchaguzi wa ndani, hivyo anaamini bado kinaendelea kujifunza
katika masuala hayo.
Alisema
kuna mambo yanaonyesha wazi kuwa katika kipindi hiki nchi inajaribiwa,
hivyo busara za viongozi zinahitajika ili kuweza kuivusha nchi salama
na watu waishi vizuri baada ya uchaguzi.
Alisema
vijana pia wana nafasi kubwa ya kupaza sauti ili kupata viongozi bora,
ikiwa pamoja na kuuliza maswali kuhusu hatima ya nchi badala ya
kushabikia.
Mmoja
wa wanafunzi alimuuliza endapo atakuwa rais atafanya nini ili Ikulu
isiwe pango la walanguzi, lakini alijibu hawezi kuongelea masuala ya
siasa katika eneo la taaluma.
“Nisingependa
katika mazungumzo haya kusema nitafanya nini nikichaguliwa ili
mnichague, swali linaloelekeza huko sitojibu, tusifanye siasa kwa sababu
hii ni sehemu ya taaluma, kama unataka mambo hayo nitafute mtaani au
katika mitandao,” alisema January.
Pia
aliitaka Tume ya Uchaguzi (NEC) kuharakisha mchakato wa uandikishaji
wapiga kura ili kuhakikisha watu wanapata haki ya kupiga kura.
Alisema
hatafurahi kuona mtu anashindwa kupiga kura kwa sababu za
kutojiandikisha, badala yake asiyepiga kura awe ni kwa sababu zake
binafsi.
22:14
Unknown
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Kaskazini, kimemchagua
Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Godbless Lema, kama Kamanda wa
Operesheni ya Uandikishaji wa Daftari la Wapigakura katika kanda hiyo.
Hayo
yalisemwa juzi jijini hapa na Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Calist
Lazaro, alipokuwa akizungumza katika kikao maalumu cha mkakati
kilichowashirikisha viongozi wa Wilaya ya Arusha, wenyeviti wa kata na
viongozi wa Chadema wa Serikali za Mitaa kutoka kata 25 za Jiji la
Arusha.
“Tuweke
akili zetu kwenye BVR kwani hakuna ushindi bila watu kujiandikisha,
naomba nimtambulishe Lema kama Kamanda wa Operesheni ya BVR katika Kanda
ya Kaskazini, ambaye ataongoza kampeni hiyo ya kuhamasisha wananchi
wajiandikishe kwa wingi ili tuweze kushinda,”alisema Lazaro
Alisema
kutokana na uhamasishaji wa Lema ambaye pia ni Mbunge wa Arusha Mjini,
utakiswezesha chama hicho kushinda katika uchaguzi mkuu na hata kuongeza
idadi ya majimbi kutoka mawili ya sasa.
Awali
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Arusha, Derick Magoma, alisema lengo la
kikao hicho ni mkakati ya kuhimiza wananchi kujiandikisha kwenye
daftari hilo ili kushinda katika uchaguzi huo kwa kishindo.
“Tusipojiandaa
sasamhatutaweza kushinda uchaguzi huu,kwani tumedhamiria kushinda kwa
kishindo, ndiyo maana tumeitana hapa kupanga mikakati ya ushindi ikiwa
ni pamoja na kuhamasisha wananchi kujiandikisha, mwaka huu hata walete
magari yenye maji ya kuwasha, mabomu, lakini ushindi ni lazima,”alisema
SOURCE MPEKUZI
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Tuko Live Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma Katika Mkutano wa Mwigulu Nchemba kutangaza nia ya Urais .
10:24
Unknown
Sasa
ni zamu ya Mwigulu Nchemba kutangaza nia ambapo tayari amewasili
katika ukumbi wa Mwl. Nyerere katika chuo cha mipango Dodoma ili
kutangaza nia yake ya kugombea Urais kwa tiketi ya Chama cha
Mapinduzi, CCM.
Hapa nimekuandikia pointi muhimu anazotoa Mwigulu Nchemba (Zinaanzia chini kuja juu);
25:
Mh. Mwigulu tayari amemaliza kuzungumza na sasa anaendelea kufurahi na
watu walioko ukumbini. Kinachofuata kwa sasa ni maswali mbalimbali
ambayo ataulizwa na kuyajibu.
24: Mambo matatu ninayowaomba Watanzania ni kwamba mniamini, pili mniunge mkono na tatu nitawavusha.
23: Natangaza rasmi kuomba ridhaa ya kugombea katika chama changu ili niweze kuleta mabadiliko Katika Nchi yangu.
22: Napoenda kupigana vita hii siendi kupigana kwaajili ya Watanzania ila mimi mwenyewe maana umaskini unanigusa.
21: Ukiwaondoa vijana mjini wakati wakifanya kazi halali kwa kigezo cha uchafu,watarudi mjini na kufanya kazi haramu.
20: Tunaposimamia kuacha kufanya kazi kwa mazoea ndio tunasema mabadiliko ni vitendo na wakati ni sasa.
19: Ninapotangaza nia ya jambo hili nimetathimini vya kutosha na nikajiridhisha na ahadi yangu ni kwamba nitawavusha.
18: Nawaambieni nawaomba kazi hii nikiwa bado nina nguvu ili niweze kufika mwenyewe maeneo yenye migogoro ya ardhi.
17: Tutasimamia Muungano wetu maana sio wa vitu ila ni watu. tutahakikisha uchumi wa Zanzibar nao unapewa kipaumbele.
16: Mtu anayeiba dawa ambazo zingemtibu maskini huyo ni mhujumu, tutamnyang'anya leseni yake na atakwenda jela.
15: Ninaposema kukomesha rushwa nitazingatia maslahi ya Wafanyakazi, haiwezekani wengine Wale kidogo na wengine kubwa .
14: Mtu anabakiza muda mchache hadi anakuja kustaafu unamuongezea muda tena kazini wakati kuna vijana wasio na kazi.
13: Mtu yoyote akithibitika amefanya vitendo vya rushwa, atafilisiwa, atafukuzwa kazi na atafungwa.
12: Rushwa hupofusha macho ya wenye akili na rushwa hurudisha nyuma maendeleo.
11: Awamu ya 5 nataka kuona nchi ikiingia kwenye uchumi wa viwanda na vijana wakifanya kazi kwa shift usiku na mchana .
10: Pia jambo lingine la kuzingatia ni Udhibiti wa matumizi mabaya ya fedha na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
9:Mambo ya kuzingatia ni Kila mtu kulipa kodi anayostahili na sio kukandamiza wafanyakazi na kinamama wauza vitumbua .
8:Mkataba wa Rais wa awamu ya tano ni juu kazi anazoenda kufanya na sio kazi alizowahi kufanya.
7: Faida ya kuwa kiongozi Kijana ni kuwa Unafanya kazi ukiwa na nguvu na ukimaliza unapumzika, kwahiyo unajiuliza tena hilo?
6: Kiongozi akipatikana kwa mazoea, atafanya kazi kwa mazoea. Nawaambieni tunataka tukomeshe kufanya kazi kwa mazoea
5: Kukaa sana serikalini si kigezo, unaweza kukaa sana serikalini na ukawa umesababishia hasara kubwa Taifa hili.
4: Nilipomaliza shahada ya 2 nilibeba zege na mke wangu alipika mama ntilie, natambua tatizo la ajira kwa vijana.
3: Kiongozi aliyekaa muda mrefu madarakani maana yake ni kwamba amesahau shida za wananchi.
2: Nimeamua kutangazia nia Dodoma kwakuwa ni Makao makuu ya Nchi na pia makao makuu ya chama.
24: Mambo matatu ninayowaomba Watanzania ni kwamba mniamini, pili mniunge mkono na tatu nitawavusha.
23: Natangaza rasmi kuomba ridhaa ya kugombea katika chama changu ili niweze kuleta mabadiliko Katika Nchi yangu.
22: Napoenda kupigana vita hii siendi kupigana kwaajili ya Watanzania ila mimi mwenyewe maana umaskini unanigusa.
21: Ukiwaondoa vijana mjini wakati wakifanya kazi halali kwa kigezo cha uchafu,watarudi mjini na kufanya kazi haramu.
20: Tunaposimamia kuacha kufanya kazi kwa mazoea ndio tunasema mabadiliko ni vitendo na wakati ni sasa.
19: Ninapotangaza nia ya jambo hili nimetathimini vya kutosha na nikajiridhisha na ahadi yangu ni kwamba nitawavusha.
18: Nawaambieni nawaomba kazi hii nikiwa bado nina nguvu ili niweze kufika mwenyewe maeneo yenye migogoro ya ardhi.
17: Tutasimamia Muungano wetu maana sio wa vitu ila ni watu. tutahakikisha uchumi wa Zanzibar nao unapewa kipaumbele.
16: Mtu anayeiba dawa ambazo zingemtibu maskini huyo ni mhujumu, tutamnyang'anya leseni yake na atakwenda jela.
15: Ninaposema kukomesha rushwa nitazingatia maslahi ya Wafanyakazi, haiwezekani wengine Wale kidogo na wengine kubwa .
14: Mtu anabakiza muda mchache hadi anakuja kustaafu unamuongezea muda tena kazini wakati kuna vijana wasio na kazi.
13: Mtu yoyote akithibitika amefanya vitendo vya rushwa, atafilisiwa, atafukuzwa kazi na atafungwa.
12: Rushwa hupofusha macho ya wenye akili na rushwa hurudisha nyuma maendeleo.
11: Awamu ya 5 nataka kuona nchi ikiingia kwenye uchumi wa viwanda na vijana wakifanya kazi kwa shift usiku na mchana .
10: Pia jambo lingine la kuzingatia ni Udhibiti wa matumizi mabaya ya fedha na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
9:Mambo ya kuzingatia ni Kila mtu kulipa kodi anayostahili na sio kukandamiza wafanyakazi na kinamama wauza vitumbua .
8:Mkataba wa Rais wa awamu ya tano ni juu kazi anazoenda kufanya na sio kazi alizowahi kufanya.
7: Faida ya kuwa kiongozi Kijana ni kuwa Unafanya kazi ukiwa na nguvu na ukimaliza unapumzika, kwahiyo unajiuliza tena hilo?
6: Kiongozi akipatikana kwa mazoea, atafanya kazi kwa mazoea. Nawaambieni tunataka tukomeshe kufanya kazi kwa mazoea
5: Kukaa sana serikalini si kigezo, unaweza kukaa sana serikalini na ukawa umesababishia hasara kubwa Taifa hili.
4: Nilipomaliza shahada ya 2 nilibeba zege na mke wangu alipika mama ntilie, natambua tatizo la ajira kwa vijana.
3: Kiongozi aliyekaa muda mrefu madarakani maana yake ni kwamba amesahau shida za wananchi.
2: Nimeamua kutangazia nia Dodoma kwakuwa ni Makao makuu ya Nchi na pia makao makuu ya chama.
1: Namshukuru MUNGU kwa kuniwezesha leo kusimama mbele yenu kwaajili ya kutangaza jambo kubwa kwaajili ya nchi yetu .
Source Mpekuzi
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
10:18
Unknown
- Nianze
kwa kutoa shukrani kwenu wote mlioacha shughuli zenu ili kuja hapa
kunisikiliza. Kuja kwenu hapa kwa wingi ni ishara ya imani mliyonayo
kwangu, Nawashukuru sana
- Kwa
zaidi ya mwaka mzima, kumekuwepo na miningo’no kuhusu uwezekano
wangu kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Aidha
kutokana na mijadala ya wananchi au kupitia mitandao ya kijamii au
vyombo rasmi vya habari, mining’ono hiyo imefanya baadhi ya watu
wanifuate ili wanishauri nigombee na wengine wamenipigia simu kwa
kunishawishi nisisite kugombea
- Leo, nakuja hapa Mwanza kuvunja ukimya na kumaliza minong’ono kwa kutangaza rasmi kwamba nimekata shauri kugombea nafasi ya urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
KWANINI NAGOMBEA
Zikosababu kadhaa, ambazo zimenisukuma kugombea kufikia uamuzi huo
- Haki
yangu ya kikatiba. Hii ni sababu ya msingi lakini siyo yenye uzito,
kwa vile ni haki ya kikatiba na ni kwa ajili ya watanzania wote.
Hivyo zinahitajika sababu za ziada licha ya haki ya kikatiba
- Naifahamu
Tanzania, Kwa muda mrefu tangu miaka ya 1970 nimeshirikishwa katika
uongozi wa nchi yetu tangu nikiwa na umri wa miaka wa 27
- 1970 kwa mara ya kwanza nilichaguliwa kuwa mbunge wa Mwibara katika wilaya ya Bunda
- 1973 niliteuliwa kuwa waziri mdogo (Juniour Minister)
- 1975 Niliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na katibu wa TANU wa mkoa
- 1982-1985 Afisa mwandamizi mkuu ubalozi wa Tanzania Marekani
- 1987-1989 Raisi alniteua kuwa naibu waziri wa serikali za mitaa na mifugo na vyama vya ushirika
- 1989-1990 Niliteuliwa kuwa Waziri wa kilimo, mifugo
- 1990-1991 Mkuu wa mkoa wa pwani na katibu wa CCM Mkoa
- 2005-2015
Waziri wa wizara ya maji , kilimo, ofisi ya Waziri mkuu Kilimo
tena Ofisi ya rais mahusiano na uratibu na hatimae kilimo tena hadi
sasa
Shughuli hizi
chini ya Marais wa awamu zote nne umenipa uzoefu mkubwa wamasuala ya
kitaifa na kuniwezesha kuifahamu vema Nchi yetu. Mimi nimiongoni mwa
Watanzania wachache, wanaoijua Tanzania ya leo nakubashiri Tanzania ya
kesho.
Kama mwanafunzi
mzuri wa nafasi mbalibali, walioniundisha waliozingatia hazina ya
uzoefu, naamini uzoefu niliopata utanisaidia sana katika uongozi wa nchi
yetu iwapo chama changu kitanipendekeza na hatimayekuchaguliwa na
watanzania kwa Rais wa nchi yetu
Pamojana yote
hayo haitakuwa rahisi kwangu kufanya uamuzi wa kugombea nafasi ya
urais.
Hii ni kwa sababu natambua majukumu na wajibu wa Rais ulivyo mzito wa kuongoza watanzania karibu million hamsini (50)na zaidi kwa ulinzi wa matumaini na matamanio yao ya nyakati.
Hii ni kwa sababu natambua majukumu na wajibu wa Rais ulivyo mzito wa kuongoza watanzania karibu million hamsini (50)na zaidi kwa ulinzi wa matumaini na matamanio yao ya nyakati.
Hata hivyo,
baada ya tafakuzi nimeridhika kuwa uamuzi wa kugombea nafasihii ya juu
kabisa katika nchi yetu ni sahihi na ni wakati mwafaka nahali ya
kisiasa ilivyo kwa sasa, najiona kuwa mtu sahihi , kwa kuwaninayo nia ya
kuipeleka nchi yetu katika ngazi ya juu zaidi kisiasa,kiuchumu na
kijamii.
SERAYA JUMLA ZA NCHI
Baadaya maelekezo hayo ya utangulizi, sasa nizungumzie mambo ya msingi nahazina yanayohusu uongozi wa nchi yetu.
Endapo nitateuliwa
na chama changu na kupata ridhaa ya watanzania na hivyokuchaguliwa
kuwa Rais wa Jamuhuri yaMuungano wa Tanzania nitaelekezanguvu zangu
katika kusimamia yafuatayo;-
- Tanzania inabaki kuwa nchi imara yenye Umoja, Amani na Mshikamano.
- Taasisi
nzito hususani mihimili mitatu ya dola ya kitaifa ( Serikali,
Mahakama na Bunge) Zinaimaimarishwa na kuwezeshwa ili zitekeleze
majukumu yake sahihi kwa mujibuwa katiba
- Utumishi wa umma utafanyiwa marekebisho ili utekeleze wajibu wake kwa uadlifu na waladi
- Kusimamia
na kuhakikisha uchumi wa nchi unaendelea kukua kwa viwango vya juu
zaidi ( kufikia tarakimu mbili) na utengenezaji wa nafasi za ajira
unaoendana na matamanio ya wananchi
- Kuhakikisha raia wa Tanzania (wazawa) Wanawezeshwa ili washiriki kikamilifu katika kuendesha uchumi wa nchi yao.
CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI TANZANIA NA WATAZANZANIA
Haitoshikuifahamu
Tanzania kama nchi na historia yake bila kuelewa changamotochangamoto
zinazowakabili wananchi. Iwapo Chama change kitaniteuakupeperusha
bendere ya CCM, na kupata ridhahaa, yako mambo manneambayo
yatashughulikiwa na serikali ya awamu ya tano chini ya uongoziwangu.
Mambo hayo ni;-
- Umasikini wa kipato
Pamoja na
mafanikioya kukua kwa uchumi na ungezeko la huduma za kijamii
yaliyopatikanakatika awamu ya nne, bado ipo changamoto kubwa ya
umasikini.
Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa asilimia 28.2 ya watanzania
ni masikini.Kwa mujibu wa takwimu hizo, wananchi wanaokabiliwa na
umasikini huo,wengi wao wananishi vijijini na kujishughulisha na kilio,
ufugaji nauvuvi.
Uduni wa maisha ya vjijini unaotokana na hali hiyo
yaumasikini ni chanzo pia cha umasikini wa mijini. Vijana wengiwanahama
vijijini kwenda mijini na hivyo kuongeza kundi la umasikiniwa mijini.
LAZIMA TUWEKEZEKATIKA KILIMO
Njia pekee
yakupambana na umasikini wa kipato hususani kwa wananchi wa vijijini ,ni
lazima tuwekeze katika sekta ya kilimo, inayojumuisha kilimomazao,
ufugaji na uvuvi. Serikali chini ya uongozi wangu, itatiliakipaumbele
cha juu katika mapinduzi ya kiimo na uchumi wa vijijiniambao utaleta
mabadiliko katia maisha ya watanzania walio wengi.
Kwa
kuzingatia uwezekano mkubwa ambao Tanzania inao katika kilimo na idadi
kubwa ya watu wanaoishi vijijini (70% - 75%) ambao wanaendesha maisha
yaokutokana na kilimo na shughuli za kiuchumi wa vijijini,
uendelezajiwake utapewa nafasi zaidi katika kuleta mabadiliko na kujenga
uwezoambao baadae unaweza kuenezwa katika sekta nyingine.
Mbinuzitakazotumika katika kuboresha kilimo ni pamoja na
- Matumizi ya sayansi ya kilimo (kiimo cha kisasa na cha kibiashara)
- Utafiti wa huduma za ugani
- Kuboresha miundombinu ya vijijni hususani barabara, umeme, na umwagiliaji.
- Upatikanaji wa mikopo katika kilimo ili kubadilisha zana, hususan kuachana na jembe a mkono hatua kwa hatua hatimaye kuweka jembe la mkono katika makumbusho ya Taifa.
- Kuongeza thamani ya mazao ya kilimo kwa kuhusisha kilimo na viwanda.
- Kuwapatia wakulima masoko ya uhakika kwa mazao yao.
MIFUGO
Maendeleo ya
mifugoyatazingatiwa ili kufanya tasnia hiyo iongeze uzalishaji na
kuwabiashara ya kuaminika, kwa kuwekeza mipenyo ya matumizi ya ardhi
ilikuhakikisha uzalishaji zaidi na ongezeko la thamani ili
kuimarishamaisha ya wafugaji, Serikali yangu itaweka kipaumbele
katikakusimamia matumizi ya ardhi hususan kutatua migogoro ya wafugaji
nawakulima kwa ufupi yafuatayo yatatiliwa mkazo;-
- Kupima ardhi kwa nia ya kuwapatiawafugaji malisho ya mifugo yao.
- Kujenga malambo / mabwawa ili kuwapatia wafugaji maji hususani katika maeneo ya mifugo yao.
- Kuwapatia vikundi vya wafugaji mikopo kwa kutumia hati ardhi kama dhamana.
UVUVI
Uvuvi una
uwezekanomkubwa wa kukua kwa kuzingatia Pwani kubwa, maziwa na mito
ambayoTanzania imejaliwa. Serikali itaweka dhamira ya kuleta
mabadilikokatika sekta hii ili iwe biashara yenye tija katika
kuongezauzalishji zaidi na kuongeza kipato ch wavuvi.
Mkazo utakuwa zaidikatika kuimarisha vitendea kazi, kupanua masoko na kuhamasishauongezaji wa thamani kwa mazao ya uvuvi.
HATUA ZAKUCHUKUA.
Kwaujumla hatua zifuatazo zitachukuliwa;
- Kuhamasisha kilimo cha ufugaji na uvuvi wa kisasa na kibiashara kwa
- Kutumia maarifa ya kisayansi
- Zana za kisasa (kuweka jembe la mkono katika makumbusho)
- Mikopo na bajeti
Kuongeza uwekezajikwa njia ya
- Bajeti ya serikali ili kugharamia elimu ya wakulima, wafugaji na wavuvi
- Utafiti na uzalishaji wa mbegu za mifugo kilimo na mabwawa ya samaki
- Miundombinu ya umwagiliaji
- Mikopo
Mikopo toka benki yaKilimo Na Benki ya Raslimali
AJIRA KWAVIJANA NA MAENDELEO YA VIWANDA
Sualala
ukosefu wa ajira kwa vijana ni kubwa kwa mujibu wa takwimu katikawizara
ya kazi, vijana milioni moja wanaingia katika soko la ajiranchini kila
mwaka kati ya hao ni vijana 200,000 tu ndio wanaopatakazi. Huu ni
uwiano mbaya sana ambao kama hatushughulikiwa unawezakusababisha
matatizo ya kijamii na kisiasa
Serikalinitakayoendesha
itaweka dhamira ya kukabili changamoto hii ya ajirakwa kutazama zaidi
ya ajira rasmi ili kujumuisha kujiajiri naongezeko la tija katika
uzalishaji ili jujipatia kipato stahiki.
Katika kipindi
chamiaka mitano ijayo, zitaendelezwa kitihada za kupata ufumbuzi
wakupunguza tatizo la ajira nchini. Kipaumbele kitakuwa katika kukuzana
kuanzisha viwanda vilivyo na uwezo wa kuajiri watu wengi kama vilevya
nguo(Pamba), Korosho, Ujenzi na vyenye kuzalisha bidhaazanazotuwa na
watu wengi wa ndani na nje.
Katika kipindi
chamiaka mitano, serikali itahakikisha sekta za uzalishaji mali ,
kamavile kilimo, ufugaji, uvuvi , viwanda vikubwa vikubwa na vidogo
nahuduma za kiuchumi kama mishati , uchukuzi na ujenzi
vinatekelezamipango yao katika kupunguza umaskini na kuzaliza ajira
Katika miaka
yakaribuni vijana wameonyesha uwezo mkubwa wa kubuni ajira nakujiajiri,
hatua ambazo zinastahili kupongeza kutiwa moyo na kuwezamfumo ya
kuwawezesha.
Ajira katika tasnia zilizokuwa kwa haraka nikatika masuala
ya mitindo, miziki na filamu kama kina diamondplatinamz , Banana zoro
na Binti yangu lady Jay dee, ommy Dimpoz,Christian Bella.
Wabunifu wa
mitindo kama vile Mustafa Hasani, AsiaIdarous, Filamu kama kina marehemu
Stephen kanumba na Mtitu Gama.Leohii tasnia hizi zinaajiri mamlioni ya
vijana.
Vijana
mafundiwanatengeneza ajira katika Nyanja za ufundi, Viko viwanda
visivyorasmi katika kila mji, kama uundaji bidhaa za vyuma, Ufundi
bomba,Useremara, Ufundi umeme na umakenika wanatoa huduma kwa maelfu
yawateja.
Katika jiji la DSM mfamo gerezani na Tabata dampo na
hapaMwanza makoroboi. Vijana wanajiajiri katika teknolojia mpya
hasaTEHAMA. Wanaunda mifumo ya kusisimua ya kumpyuta na hata simu
zamkononi na kumuwezesha mtumiaji kutatua matatizo mbalimbali.
Vijana na mifumo yausafiri wa umma kwa kutumia baiskeli, pikipiki na pikipiki za miguumitatu zimeongeza ajira.
Wafanyabiasharamaarufu
kama wamachinga, hawa huuza chochote unachohitaji, kuanziamagazeti na
mahitaji mengine.
Kundi hili linahitaji kuwekewa mipangokwa kutengewa
maeneo ya biashara badala ya kukamatwa kamata kilakukicha. Mama ntilie
ni kundi linalotoa huduma muhimu ya chakula hasamijini.
Source mpekuzi
TOA MAONI YAKO HAPA LAKINI MATUSI HAPANA .
Subscribe to:
Posts (Atom)