Haris Suleman na baba yake mzazi ambae pia ni Rubani walichukua mafunzo mbalimbali ya kutua kwenye maji wakati wa dharura kabla ya kuanza safari yao waliyoiandaa kwa miezi wakiwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto wa familia masikini nchini Pakistan waweze kwenda shule.
Sasa imethibitika kwamba mtoto huyu rubani aliekua anataka kuweka rekodi ya dunia kwa kuwa rubani mdogo aliesafiri umbali mrefu, amefariki dunia na mwili wake kupatikana baada ya ajali ya ndege hiyo iliyotokea baharini Jumanne usiku ambapo Baba yake ambae walikua pamoja hajulikani alipo.
Mpaka sasa chanzo cha kuanguka kwa ndege hii hakijajulikana ambapo Hiba Suleman ambae ni dada wa marehemu amesema ‘tunatumai baba yetu yu hai, tutaendelea kusali mpaka tutakapopata jibu la mwisho… ‘
Wawili hawa walikua na blog yao ambayo walikua wanapost vitu mbalimbali zikiwemo picha za wanakopita au kutembelea ambapo post yao ya mwisho kuiweka ilikua ni July 20 2014 Bali Indonesia.
Ahmed amesikitishwa na ajali waliyoipata na kusema imeuma zaidi hasa kwa sababu ndio ilikua karibu wamalize safari hii ambayo ni rekodi ya dunia.
0 comments:
Post a Comment