Thursday, 31 July 2014

Hatimaye Romelu Lukaku amebebwa rasmi na Everton kwa kitita cha pauni milioni 28. Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji mwenye miaka 21 aliyefunga mabao 16 akiwa Everton kwa mkopo msimu uliopita sasa atatumika pale Goodison Park kwa miaka mitano. Bosi wa Everton Roberto Martinez amsemea: "Usajili huu sio tu muhimu kwa msimu huu, ni siku muhimu katika historia ya klabu." Lukaku alijiunga...
Mabingwa wa Spain, Atletico Madrid wanataka kuwasajili Santi Cazorla, 29, kutoka Arsenal, Fernando Torres, 30, kutoka Chelsea na Chicharito, 26 kutoka Manchester United (Daily Star), Chicharito amekiri kuwa hana uhakika kama ataendelea kuwepo Old Trafford akisema "Mungu pekee ndio anajua" kuhusu hatma yake (Guardian), Tottenham wanatarajia kurejea na fedha zaidi kumtaka kiungo...
Bi. Nasra Dafa (30) aliyeshambuliwa na mume wake wakati akiswali.TUHUMA nzito ya aina yake ambayo haijawahi kutokea ambapo mkazi mmoja wa Tandale – Kwatumbo wilayani Kinondoni jijini DAR, Idd Mpenda anadaiwa kumshambulia na kumjeruhi hadi kuzimia mkewe, Nasra Dafa (30) wakati akiswali.Akizungumza na Amani huku akimwaga machozi, mwanamke huyo alisema tukio hilo lilijiri Julai 28, mwaka huu...
Mbunge wa Vunjo, Augustino Mrema (TLP) amesema amejiandaa kuingia ‘vitani’ na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ambaye ametangaza kuwania ubunge katika jimbo hilo, mwaka 2015.“Siogopi mtu yeyote. Nimejiandaa vilivyo kwa mpambano huu. Najivunia rekodi yangu nzuri ya utendaji wala sitishiki na wananchi wangu nimewauliza wameniambia nisihofu,” alisema Mrema.Kwa mujibu wa Mrema, anaamini...
Taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa mbeya kwa vyombo vya habari “press release” tarehe 31.07.2014.    Watu wanne wafariki dunia na wengine 51 kujeruhiwa katika ajali ya gari matundasi wilayani chunya.    Mtu mmoja afariki dunia katika ajali ya barabarani jijini mbeya.    Mtoto wa miaka mitatu afariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi cha mchanga...

Wednesday, 30 July 2014

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa mara nyingine ametunukiwa tuzo la kimataifa – zamu hii kwa kuwa mshindi waTuzo la Nyota wa Demokrasia Afrika  2014 – Icon of Democracy Award Winner for 2014 in Africa.Kwa mujibu wa barua aliyoandikiwa Rais Kikwete na kupokelewa Ikulu, Dar Es Salaam, Rais Kikwete amekuwa mshindi wa kwanza, na kwa mbali...
  Takribani watu 20 wanadaiwa kupoteza maisha huku wengine wengi wakijeruhiwa baada ya basi la Moro Best lililokuwa linatoka Mpwapwa kwenda Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na lori eneo la Pandambili, Kongwa mkoani Dodoma leo. Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Mkoa Dodoma huku wengine wakipelekwa Hospitali ya Mpwapwa. ...
Ziwa Nyasa limezungukwa na nchi tatu ambazo ni Tanzania,Malawi na Msumbuji.Ziwa hilo lipo kwenye usawa wa meta 500 toka usawa wa bahari, kina cha ziwa hilo ni karibu meta 750,urefu wake ni karibu  kilometa 1000,upana mkubwa ni kilometa 80 na upana mdogo ni kilometa 15.Huku tafiti mbalimbali zikionesha kuwa ziwa hulo ndilo zuwa pekee linaongoza kwa aina za samaki ,na kutokana na utafuti ambao...
Shinji Kagawa, Darren Fletcher na Tom Cleverley, wafungaji wanne wa penati za United, wakishangilia ushindi wao wa penalti 5-3 dhidi ya Inter Milan. Fletcher akishangilia ushindi na kipa wa United David De Gea baada ya kushinda kwa penalti na kumpa Van Gaal rekodi ya ushindi wa asilimia 100 katika michuano hiyo. KOCHA Louis van Gaal ameendelea kufanya vizuri kufuatia Manchester United...
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 30.07.2014 [BARAKAEL .N. MASAKI – ACP] MZEE WA MIAKA 75 AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA.  KATIKA TUKIO LA KWANZA:  MZEE MMOJA MWENYE UMRI WA MIAKA...
...
Mrembo almaarufu kwa jina la 'Winnie Mandela' katika muziki wa kizazi kipya akiwa amenaswa na polisi China.HUKU modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’, akisota jela nchini China kwa skendo ya kukamatwa na madawa ya kulevya (unga), mrembo mwingine ambaye aliwahi kujaribu kuchomoka kisanii kwenye muziki wa Kizazi Kipya almaarufu kwa jina la Winnie Mandela, naye...
Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Ubungo, Goodluck JustineUONGOZI mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya kichama Ubungo unatarajiwa kujulikana Agosti 3 mwaka huu baada ya uchaguzi wa ngazi za chini katika wilaya hiyo kukamilika.Mbali na viongozi wa wilaya hiyo kujulikana siku hiyo, pia chama hicho kimeeleza kuwa, kimejiandaa vema kuwadhibiti mamluki wasijipenyeze katika uongozi...
...