Friday, 19 September 2014

Katika hali isiyotarajiwa, mwanafunzi wa Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Ezra Gerald (19), amejinyonga hadi kufa kwa kutumia shuka ya hospitali, alikokuwa amelazwa kwa kile kinachoeleza alikuwa anasumbuliwa na homa ya matumbo.

Hata hivyo, ujumbe ulioachwa na marehemu huyo unaonesha alichukua uamuzi huo, kutokana na kuchukizwa na uamuzi wa daktari aliyemhudumia wa kumlaza ili atibiwe ugonjwa ambao hakuwa anaumwa.

Aidha, katika ujumbe huo imeelezwa alichukizwa na kitendo cha kupotezewa muda hospitalini wakati wenzake wakiendelea na masomo.

Tukio hilo limethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Gilles Muroto aliyesema mwanafunzi huo alijinyonga Septemba 16 mwaka huu saa moja asubuhi.

Alisema mwili wake uligundulika ukining’inia kwenye mti uliopo maeneo ya hospitali hiyo na alipopekuliwa katika mifuko ya suruali yake, zilionekana karatasi mbili, moja ikiwa na ujumbe uliosomeka; “Haiwezekani binadamu kuhudumiwa kama mbwa, yaani nafika hospitali najieleza hali yangu halafu daktari ananiandikia kulazwa bila kupima, sasa sijui wanatibu nini?

“Kwa kweli siwezi kuvumilia wenzangu wanasoma halafu mimi nimekalishwa tu hapa hospitali bila kujua wananitibu nini, inaniuma sana mpaka nafikia hatua hii ya kujiondoa duniani kwa sababu naona watu wanachezea ndoto zangu, mimi siwezi kuona ndoto yangu inazimwa wakati natakiwa niwepo shuleni nikamilishe ndoto zangu “mjitahidi tukutane mbinguni “Respect My Family and Brother Henry.”

Kamanda Muroto amesema hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo, lakini polisi wanaendelea na uchunguzi.

Inaelezwa mwanafunzi huyo aliyetajwa kuwa ni mwenyeji wa mkoa wa Tabora, alilazwa hospitalini hapo tangu Septemba 11 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Katibu wa Hospitali ya Mkoa wa Kagera, Benges Justus, tukio hilo lilitokea Septemba 16, mwaka huu, siku moja baada ya mgonjwa huyo kulazwa.

Alisema baada ya mwanafunzi huyo kupokelewa hospitalini hapo, alifanyiwa vipimo vyote vya kitabibu na kugundulika anasumbuliwa na malaria, ndipo akaanzishiwa tiba ya ugonjwa huo.



Siku chache baada ya majambazi kuvamia Kituo Kikuu cha Polisi wilayani Bukombe mkoani Geita, kuua askari wawili na kuiba silaha za moto, watu wasiofahamika wamewajeruhi askari watatu waliokuwa doria kwa kuwarushia kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu.
 
Askari hao kwa sasa wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea wakitibiwa majeraha.

Tukio hilo limeripotiwa kutokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa moja na nusu jioni katika kata ya Msufini karibu na daraja la Matarawe, wilayani Songea.

Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI), Issaya Mngulu amethibitisha kwa njia ya simu kutokea kwa tukio hilo, ingawa alishindwa kuingia kwa undani akisema alikuwa njiani kwenda eneo la tukio akitokea mkoani Mbeya.

Hata hivyo, kwa  mujibu wa ripota  wetu  toka  eneo  la  tukio  ni  kuwa, waliojeruhiwa  ni WP. 10399 PC Felista aliyejeruhiwa mguu wa kulia  kwenye unyayo na pajani, G 7351 PC Ramadhani aliyejeruhiwa mguu wa kulia karibu na goti na tumboni upande wa kulia na G. 5515 PC John aliyepata majeraha katika mguu wa kulia chini ya goti na jeraha dogo tumboni.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Dk Daniel Malekela, akizungumzia tukio hilo alikiri kupokea majeruhi na kueleza kuwa ametoa vipande vya bati na misumari katika majeraha ya askari hao na mpaka sasa wanaendelea na matibabu.
 

Habari zaidi zinasema jeshi la polisi mkoani humo kwa kushirikiana na maofisa wengine kutoka makao makuu ya jeshi, wanaendelea na uchunguzi, ikiwa ni pamoja na kujua chanzo cha tukio hilo. Bomu hilo la kutupwa kwa mkono inasadikiwa limetengenezwa kienyeji.

Kutokana na tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Saidi Mwambungu ameelezea kusikitishwa na kitendo hicho cha wahalifu kujeruhi askari kwa makusudi na amesema Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama itahakikisha wanawasaka na kuwakamata.
Askari Polisi wakiwa eneo la tukio kuimarisha ulinzi
Eneo la tukio  likiwa limezungushiwa alama na Jeshi la Polisi. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwangu akizungumza jambo  katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma baada ya kuwatembelea majeruhi hao. Kamati ya ulinzi na Usalama wakiwa Hospital ya mkoa wa Ruvuma. Aliye lala kitandani ni WP ambaye amejeruhiwa akiwa amelazwa katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr Daniel Malekela akizungumza na waandishi wa habari hopitalini hapo. Askari Ramadhani Ally akiwa anaelezea jinsi mkasa huo ulivowakuta wakiwa kazini

Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Mh. Patrick Tsere Akizungumza na waandishi wa Habari kutoka Mbeya walipotembelea Ofisi za ubalozi Nchini Malawi 
Baadhi ya Waandishi wakimsikiliza Balozi 
 Baadhi ya Waandishi wa Habari Kutoka Mkoani Mbeya wakimsikiliza Balozi kwa Makini
 Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Mh. Patrick Tsere akipokea Taarifa kutoka kwa waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya 
 Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Mh. Patrick Tsere akijibu Taarifa ya waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya .
Waziri wa Habari , Utalii na Utamaduni Nchini Malawi Mh. Kondwani Nankumwa akiongea na waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya Ofisini kwake.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya wakifuatilia Hotuba ya Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni Mh. Kondwani Nankumwa
 Wa kwanza Kulia ni Afisa Habari wa Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni akifuatilia Mkutano huo
 Waandishi wa Habari wakiendelea kufuatilia Kikao hicho
Francis Phiri wa kwanza Kulia ambaye ni Mratibu wa ziara hiyo Nchini Malawi na Muasisi wa Nyika Press Club ya Malawi akiwa katika Mkutano huo.
Kikao kikiwa Kinaendelea 
Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni Nchini Malawi  Mh. Kondwani Nankumwa wa pili kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari Kutoka Mkoa wa Mbeya nje ya Ofisi yake Jijini Lilongwe.


Waziri wa Habari,Utalii na
Utamaduni nchini Malawi Mheshimiwa Kondwani Nankhumwa alisema kuwa Serikali ya
Malawi haina mgogoro na Serikali ya Tanzania kuhusiana na mpaka wa ziwa Nyasa.
 
Aliyasema hayo baada ya
kukutana na Jopo la Waandishi Habari wa Mkoa wa Mbeya waliotembelea ofisini
kwake katika mfululizo wa ziara ya waandishi waliofanya ziara ya juma moja
nchini humo katika ziara ya kubadishana uzoefu baina ya Waandishi wa Nchi hizo.
 
Waziri Nankhumwa alisema  kuwa Mtoto wa Rais  wa Malawi Profesa Ather Muthalikana  anasoma Dar es Salaam naye Rais amekuwa
Muhadhiri wa chuo kikuu na kwamba Watanzania wengi wanaishi na kufanya biashara
nchini Malawi hivyo hakuna sababu za kuwepo kwa tofauti za aina  yoyote ile itayowapelekea kuwagawa wananchi
wa pande hizo.
 
Aidha alisema kuwa ili kuonesha
hakuna tofauti baina ya wananchi wa pande hizo Marais wa nchi hizo watapaswa
kuchukua ndoano na kuvua samaki pamoja katika ziwa hilo ili kuionesha Dunia
kuwa wananchi wa pande hizo ni wamoja na kuna mwingiliano wa makabila.
 
Kauli hiyo iliungwa mkono na Balozi
wa Tanzania nchini Malawi Patrick Tsere ambaye alisema kuwa hakuna mgogoro wa
mpaka katika Ziwa Nyasa baina ya Tanzania na Malawi.
 
Aliyasema hayo alipotembelewa
na waandishi wa Habari wa Mkoa Mbeya walipotembelea ofisi ya Ubalozi wa
Tanzania nchini Malawi katika mfulizo wa ziara ya waandishi hao nchini Malawi
ili kubadilishana mawazo na changamoto mbalimbali zikiwemo za mazingira,utalii
na Elimu juu ya Ukimwi ambazo zinafanana katika nchi hizo.
 
Balozi Tsere alisema hivi sasa
si wakati wa marumbano kwani inahitajika subira katika mzungumzo yaliyonza
baina ya viongozi wa nchi hizo na kwamba si wakati wa kuupeleka mgogoro huo
katika mahakama ya  kimataifa ambapo
utazigharimu fedha nyingi nchi hizo katika utatuzi wa mgogro huo.
 
Hata hivyo Waandi wa Habari wa nchi
hizo walifanya makubaliano ambayo yatasaidia kuzitangaza nchi hizo kimataifa
ikiwa ni pamoja na mbuga za wanyama zilizopo
Malawi na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe ili utumiwe na wananchi
hizo ili kukuza uchumi wan chi hizo.
 
Katika ziara hiyo
Waandishi  wa vyombo mbalimbali
walishiriki ikiwa ni pamoja na Tone Multimedia Group, Mbeya yetu Blog,Chanel Ten,Mwananchi,Jambo leo,Bomba Fm,Majira
na Raia Mwema.
 
Vingine na Tanzania
Daima,Baraka FM na Mwandishi Rais mstaafu Ulimboka Mwakilili ambaye alikuwa
Mwenyekiti wa safari na Mhandisi wa Ujenzi Claudio  Lusimbi ambaye ni Mlezi Katika Safari hiyo
 


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa La Guardia jijini Washington DC tayari kwa kushiriki katika mikutano mbalimbali na pia katika hafla ya “USIKU WA JAKAYA”  leo jioni

 Rais Kikwete akilakiwa na maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kuwasili hoteli aliyofikia

 Karibu Washington DC Mheshimiwa

 Rais akiendelea kusalimia na na wafanyakazi wa ubalozini

 Mapokezi yakiendelea

 Rais Kikwete akisalimiana na Bw. Lucas Mkama wa Vijimambo Blog

Karibu sana Mzee…



 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid, akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo iliyomaliza muda wake na mpya wakati akizindua bodi hiyo Dar es Salaam leo asubuhi.
 Mganga Mkuu wa Serikali, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dk.Donan Mmbando akizungumza katika hafla hiyo kabla hajamkaribisha Waziri kuzindua bodi hiyo.
 Mwakilishi wa bodi iliyomaliza muda wake, Profesa .Bakari Lembaritiakitoa neno la shukurani
 Mwakilishi wa bodi mpya, Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk.Frank Lekey  akitoa neno la shukurani. Kushoto ni Naibu Msajili Hospitali Binafsi Dk.Mahewa Lusinde na Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Dk.Mpoki Ulisubisya.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid (kulia),akimkabidhi cheti cha utumishi wa bodi hiyo,Profesa Bakari Lembariti. Katikati ni Mganga Mkuu wa Serikali, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dk.Donan Mmbando. Vyeti hiyo walitunukiwa wajumbe wote waliomaliza muda wao.
 Wajumbe wa Bodi mpya wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk.Frank Lekey, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Dk.Mpoki Ulisubisya, Mwanasheria Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Onorius Njole, Mkurugenzi Association of Private Health Facilities-APHTA na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi-Hospitali za Umma na Binafsi Idara ya Tiba, Dk.Sijenunu Aaron.
 Wajumbe wa bodi iliyomaliza muda wake. Kutoka kulia ni Profesa .Bakari Lembariti, Profesa Charles Majinge, Dk.Edda Vahahula, Dk.Jane Kahabi na Dk.Eliuter Samky.
 Mkutano ukiendelea.
 Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara hiyo, Dk.Margareth Mhando na Mkurugenzi wa Idara ya Uhakiki na Ubora, Dk.Mohamed wakiwa kwenye mkutano huo.
 Katibu wa Bodi hiyo, Dk.Pamella Sawa akizungumza katika mkutano huo.(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi-Hospitali za Umma na Binafsi Idara ya Tiba, Dk.Sijenunu Aaron akiteta jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Vituo vya Umama na Binafsi na Mwakilishi wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali Binafsi Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Ruth Suza.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi iliyomaliza muda wake.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya.



SERIKALI imesema itaainisha ukomo wa tozo kwa kila huduma inayotolewa kwa kila ngazi ya kituo cha huduma ili kudhibiti gharama za huduma za afya nchini.

Kauli hiyo ilitolewa  na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid Dar es Salaam leo asubuhi wakati akizindua bodi mpya ya ushauri ya Hospitali binafsi nchini.

Dk. Rashid alisema hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa malalamiko kuhusu huduma zinazotolewa na hospitali hizo hivyo hatua hiyo itasaidia kuboresha mfumo na kuwatendea haki wananchi wanaotumia vituo  vya kutolea huduma za afya.

"Malalamiko haya ni pamoja na huduma zisizo na ubora unaotakiwa na gharama zinazotolewa kwa huduma hizo .Sheria iliyopo inatutaka kudhibiti bei ya huduma hizi kwa kuzingatia malalamiko haya pamoja na matakwa ya sheria yenyewe," alisema Dk. Rashid.

Hata hivyo alibainisha kuwa licha ya kuwepo wa changamoto hizo huduma zinazotolewa na hospitali za watu binafsi zimechangia katika mafanikio  yaliyopatikana katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.

Kuhusu bodi hiyo Dk .Rashid aliwataka wajumbe wapya wa bodi hiyo kufanya vikao vya mara kwa mara vinavyolenga uboreshwaji wa utoaji wa huduma.Na kuwataka kuendeleza utaratibu wa kusajili vituo vipya na kufupisha usajili kwa kutmia muda mfupi  kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.

Alibainisha kuwa wajumbe wa bodi ya awali iliyosimamiwa na Mwenyekiti Dk. Deo Mtasiwa imesaidia kuboresha uwajibikaji wa wahusika hivyo kuboresha huduma na imeokoa maisha ya wananchi wengi ambayo yangekuwa hatarini endapo bodi isingetekeleza majukumu yake ipasavyo.

Alitaja wajumbe wa bodi mpya kuwa ni Dk.Donan Mbando ambaye ni Mwenyekiti, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa mbeya Dk. Mpoki Ulisubisya, Mkurugenzi wa Hospitali ya Bugando Profesa Chalres Majinge, Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi (NHIF), DK. Frank Lekey.


Wajumbe wengine ni Mkurugenzi Msaidizi- Hospitali za Umma na Binafsi Idara ya Tiba Dk. Sijenunu Aaron, Mkurugenzi wa Association of Private Health Facilities (APHTA), Mwakilishi wa Mkurugenzi, Christian Social Services Comission (CSSC), Dk.Jane Kahabi na Mwanasheria Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Onorious Njole.


 
Wananchi wa Scotland waliokuwa wakitaka kujitenga na Uingereza wakiangua kilio huku walioshinda wakiwa na furaha baada ya matokeo kutangazwa. MATOKEO ya kura za maoni nchini Scotland yametoka, kura 1,914, 187 sawa na 55% wamepinga kujienga na Uingereza huku kura 1,539,920 sawa na 45% wakitaka kujitenga. 
Kwa matokeo hayo, Scotland itaendelea kuwa sehemu ya Uingereza na Waziri Kiongozi wa Scotland Alex Salmond amesema ameridhia kuanguka katika mchakato wa kura ya maoni.

 

pix 1Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo (mwenye shati la batiki), akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito wa Thailand, walipotembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya 54 ya Vito na Usonara ya Bangkok, yaliyofanyika Septemba 9 hadi 13 mwaka huu.
pix 2 
 
Makamu wa kwanza wa Rais wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito na Usonara wa Thailand, Bw. Sutipong Dumrongsakul, akimkabidhi zawadi maalumu Mkuu wa Ujumbe kutoka Tanzania ulioshiriki maonesho ya vito ya Bangkok, Archard Kalugendo, mara baada ya kikao kati ya Ujumbe huo na Viongozi wa Taasisi hiyo ya Wafanyabiashara wa Thailand.
pix 3 
Wateja mbalimbali wakihudumiwa katika Banda la Tanzania kwenye maonesho ya vito na usonara ya Bangkok yaliyofanyika hivi karibuni nchini Thailand.Baadhi ya Watanzania walioshiriki maonesho ya vito na usonara nchini Thailand, wakimsikiliza mmoja wa wateja aliyetembelea Banda la Tanzania.
pix 5 
Ujumbe wa Tanzania (Kulia) wakiwa katika kikao na Uongozi wa juu wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito na Usonara wa Thailand, ambao ndiyo waandaaji wa maonesho ya vito na usonara ya Bangkok.
pix 6 
Baadhi ya Watanzania walioshiriki maonesho ya vito na usonara ya Bangkok, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungwa rasmi kwa maonesho hayo.
pix 7Watanzania walioshiriki maonesho ya vito na usonara ya Bangkok walitumia fursa ya maonesho hayo kutangaza pia utamaduni na vivutio mbalimbali vya utalii vipatikanavyo nchini Tanzania. Pichani ni Eva Mowo (kushoto) Afisa kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Lightness Makundi, Afisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakiwa wamevalia mavazi ya kimasai.
pix 8 
Ujumbe wa Tanzania ulioshiriki katika maonesho ya vito na usonara ya Bangkok pia walitumia fursa ya maonesho hayo kutangaza maonesho ya vito ya Arusha yanayotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu jijiji Arusha. Pichani ni Eva Mowo, Afisa kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Lightness Makundi, Afisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakiwa wamepozi katika bango lenye ujumbe wa kutangaza maonesho ya Arusha. Maafisa hao walivalia mavazi ya asili (vitenge) na mikufu yenye vito vya Tanzanite kutangaza utamaduni wa Kitanzania na madini hayo maarufu ya vito yapatikanayo Tanzania pekee.  
pix 9 
Makamu wa Rais wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito – Thailand, ambao ndiyo waandaaji wa Maonesho ya Vito ya Bangkok, Tony Brooke akizungumza na baadhi ya Watanzania walioshiriki katika Maonesho hayo nchini Thailand alipotembelea Banda la Tanzania. Sambamba naye (mwenye shati la kitenge) ni Mkuu wa Ujumbe wa Tanzania katika maonesho hayo, Archard Kalugendo.
 
Tanzania, Thailand kushirikiana katika madini vito

Wafanyabiashara wa madini ya vito na usonara wa Thailand wameonyesha nia ya kushirikiana na Tanzania katika sekta hiyo kwa lengo la kukuza uhusiano na kuzinufaisha pande zote mbili.
Hayo yalibainika hivi karibuni katika kikao kilichokutanisha Ujumbe wa Tanzania ulioshiriki Maonesho ya Vito na Usonara yaliyofanyika Bangkok nchini Thailand na Uongozi wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa madini hayo kutoka nchini humo.
Akiwasilisha  maoni na mapendekezo kutoka upande wa Tanzania katika kikao hicho, Kiongozi wa Ujumbe kutoka Tanzania, Archard Kalugendo ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), alisema Tanzania inapenda kushirikiana na Wa-Thailand katika sekta hiyo ili pamoja na mambo mengine kuiga na kujifunza kutoka kwao.
“Ninyi wenzetu mmeendelea sana katika sekta hii ya madini ya vito na usonara. Tunapenda kujifunza na kuiga kutoka kwenu ili nasi tufike hapo mlipofikia na hata zaidi ya hapo,” alisema Kalugendo.
Aliongeza kwamba, lengo la Serikali ya Tanzania ni kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha inawawezesha wananchi wake hususan wanaojishughulisha na biashara ya madini ya vito na usonara ili wanufaike ipasavyo kupitia kazi hiyo na pia kulinufaisha Taifa kwa ujumla kwa kukuza uchumi wa nchi.
Alisema, Serikali inayo nia na imejipanga kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha biashara ya madini ya vito na usonara katika Bara la Afrika na kwamba inatumia njia mbalimbali kufanikisha hilo ikiwemo kuendelea kuboresha Maonesho ya Vito na Usonara ya Arusha (Arusha Gem Fair – AGF) yanayofanyika kila mwaka.
Kalugendo alitumia fursa hiyo kuwakaribisha Wafanyabiashara wa Thailand katika Maonesho ya Vito ya Arusha yanayotarajiwa kufanyika mapema mwezi Novemba mwaka huu jijini Arusha.
“Tanzania inayo mazingira mazuri sana ya uwekezaji na ninawahakikishia kuwa ushiriki wenu katika maonesho hayo utakuwa wenye tija kwenu na kwetu pia,” alisema.
Aidha, Kalugendo alitoa maombi ya Tanzania kupatiwa nafasi kubwa zaidi katika Maonesho ya Vito na Usonara ya Thailand ili washiriki wengi zaidi wakiwemo wachimbaji na wafanyabiashara wa madini hayo waweze kushiriki na kujipatia uzoefu utakaowasaidia kuboresha utendaji wao na hivyo kumudu ushindani katika soko na viwango vya kimataifa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Maonesho ya Vito na Usonara ya Arusha, Peter Pereira alisisitiza umuhimu wa Thailand kushiriki katika maonesho ya Arusha na kuwahakikishia kuwa mazingira mazuri yameandaliwa kwa ushiriki wenye tija ikiwemo kuondoa gharama za kodi ya thamani katika bidhaa (VAT) kwa kipindi chote cha maonesho.
Akijibu hoja na mapendekezo kutoka upande wa Tanzania, Makamu wa Rais wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito – Thailand, ambao ndiyo waandaaji wa Maonesho ya Vito ya Bangkok, Tony Brooke alisema Thailand inapenda kushirikiana kwa ukaribu zaidi na Tanzania katika sekta hiyo.
Alisema Wafanyabiashara wa Thailand watashiriki katika maonesho ya vito ya Arusha na kuahidi kuboresha ushiriki wa Tanzania katika maonesho ya vito ya Bangkok.
Brooke alitoa changamoto kwa Tanzania kujiandaa vema zaidi katika ushiriki wa maonesho kama hayo kwa kuhakikisha inapeleka madini na bidhaa kwa wingi kulingana na uhitaji wa wateja.
“Wateja wengi wanatembelea banda la Tanzania kuliko madini na bidhaa zilizopo. Ongezeni wingi wa bidhaa maana uhitaji ni mkubwa,” alisisitiza Brooke.
Alikubaliana na wazo la kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha madini ya vito na usonara katika bara la Afrika na kusisitiza kufanya kazi kwa bidii, weledi na kujituma kwa hali juu ili kuhakikisha lengo hilo linatimia.
“Hatua mnayoona tumefikia katika sekta hii ya madini ya vito na usonara imekuja kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na kujituma, hivyo nanyi ili mfanikiwe mnapaswa kufanya hivyo,” alisema.
Nchi ya Thailand ina uzoefu wa miaka 40 katika biashara ya madini ya vito na usonara na imekuwa ikiandaa maonesho makubwa kila mwaka katika kipindi hicho chote ili kuuza bidhaa zitokanazo na madini ya vito na kujitangaza zaidi kimataifa.
Maonyesho ya Vito na Usonara ya Bangkok kwa mwaka huu yalifanyika kuanzia Septemba 9 hadi 13 na kushirikisha mataifa mbalimbali duniani.