Monday, 22 December 2014

Masikio ya Watanzania leo yameelekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete watakapokuwa wakisikiliza hotuba yake kwa Taifa inayotarajiwa kujibu maswali yapatayo 10 ambayo yanatarajiwa kutegua kitendawili cha kashfa ya uchotaji wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow.
Maswali hayo yanatokana na maazimio ya Bunge ambayo yalionekana kuvuta hisia za wananchi katika kona mbalimbali za nchi ambako walikuwa wanafuatilia moja kwa moja mjadala wa Bunge hadi kupitishwa maazimio hayo.
Hotuba hiyo inayotarajiwa kutolewa wakati Rais atakapozungumza na wazee wa Dar es Salaam, ikiwa ni siku nne baada ya Kampuni za IPTL na Pan Africa Power Solutions (PAP) kukimbilia mahakamani kuzuia utekelezwaji wa maazimio ya Bunge.
Baadhi ya wasomi nchini wamesema hatua ya kuzuia utekelezaji wa maazimio hayo pamoja na kauli ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kuwa akijiuzulu Rais atamshangaa, ni mambo yanayofanya hotuba ya Rais kusubiriwa kwa hamu.
Swali la kwanza ambalo wananchi wanasubiri jibu lake ni iwapo Rais Kikwete atatuliza kiu yao kuhusu kashfa hiyo ambayo imekuwa gumzo nchi nzima na hivyo kulegeza msimamo wa wahisani wa kuinyima nchi misaada.
Pili, wananchi wanasubiri kusikia iwapo Rais Kikwete ataagiza uchunguzi zaidi wa Takukuru, Polisi na vyombo vingine kama ambavyo azimio la kwanza la Bunge linavyotaka wahusika wachukuliwe hatua za kisheria kuhusika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya Akaunti ya Tegeta Escrow.(MM)
Tatu, wanasubiri kwa hamu kuona hatua ambayo Rais Kikwete atachukua dhidi ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi pamoja na Profesa Tibaijuka kutokana na kutajwa katika maazimio hayo ya Bunge.
Kwa nyakati tofauti, viongozi hao wamekaririwa wakisema kuwa hawahusiki na kashfa hiyo. Mbali ya Profesa Tibaijuka kujitokeza kujitetea mwenyewe, baadhi ya wananchi wamejitokeza kuwatetea na kuwasafisha viongozi hao katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Nne, Je, atatengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme (Tanesco) ambayo pia ilitakiwa kuwajibishwa ikiwa chini ya Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Robert Mboma.
Tano, ili kuwachukulia hatua majaji waliotajwa, Aloysius Mujulizi na Profesa Eudes Ruhangisa, Rais Kikwete anatakiwa aunde Tume ya Kijaji ya kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili zinazowakabili, kinachosubiriwa kwa hamu ni kuona endapo ataunda tume hiyo.
Swali la sita linalohitaji jibu linahusu kupambana na kudhibiti vitendo vya rushwa kubwa, ufisadi na hujuma za uchumi. Kinachosubiriwa ni jibu la Rais Kikwete iwapo Serikali itaandaa na kuwasilisha muswada wa marekebisho ya sheria iliyoiunda Takukuru kwa lengo la kuanzisha taasisi mahsusi itakayoshughulikia masuala hayo.
Vilevile, wananchi wanatazamia kupata suluhisho la gharama kubwa za umeme katika jibu la Rais Kikwete iwapo Serikali iko tayari kuinunua mitambo ya Kampuni ya IPTL kama ilivyopendekezwa na Bunge kwa lengo la kuokoa fedha za Tanesco zinazotumika kununua umeme kwa bei ya juu.
WANANCHI

Friday, 19 December 2014

MKUU wa Polisi Wilaya ya Mjini, Ali Makame (wa pili kushoto) akiangalia gari iliyovunjwa na kuibiwa pesa zinazosadikiwa kuwa ni euro elfu moja na shilingi za kitanzania milioni tano, muda mfupi baada ya kufika eneo la tukio katika eneo la Mlandege mjini Zanzibar.
ASKARI Polisi wakiwa wameizunguka gari iliyovunjwa na kuibiwa pesa zinazosadikiwa kuwa ni euro elfu moja na shilingi za kitanzania milioni tano, tukio hilo limetokea majira ya saa saba mchana katika eneo la Mlandege mjini Zanzibar leo. Mmiliki wa gari hiyo aliegesha gari yake na kuingia msikitini kwa kusali sala ya Ijumaa katika msikiti jirani na maengesho ya gari katika eneo la mlandege. (Picha na Haroub Hussein).


Kwa nchi nyingi za Afrika hasa Tanzania zinapiga marufuku kubwa ya uonyeshwaji wa movie za ngono kutokana na kwamba hazina maadili mazuri kwenye jamii, ukienda nchi kama China wao wameenda mbali zaidi, sheria kali zimewekwa ili kuzuia kabisa mtu yeyote kucheza filamu hizo, ama kuuza.

Nchi za Ulaya na Marekani zimekuwa zikishutumiwa kuruhusu biashara zote, kutengeneza na kuuza movie hizo, lakini hii kutoka Los Angeles, Marekani imeweka sheria inayowalazimu waigizaji wa filamu hizo za ngono kuvaa mipira maalum ya kuwakinga na maambukizi ya magonjwa, Condom.

Sheria hii ambayo iliyoanza kama muswada mwaka 2012 inawalazimu waandaaji wa filamu hizi pia kulipia ada maalum ili kupewa kibali cha kufanyia kazi hiyo.

Waandaaji wengi wa filamu za ngono wamelalamikia sheria hii wakidai kuwa inakwenda kinyume na haki zao za msingi japo Mahakama imetoa tayari msimamo wake.

Wadau wa industry ya filamu hizo wamedai kuwa wanafahamu fika hatari zilizoko kwenye maambukizi na wanachukua hatua za kupunguza maambukizi haya kwa kuwakinga na kuwapima watu wote wanaoshiriki uigizaji wa filamu hizi kabla ya kuingia nao mikataba ambapo utaratibu huu mpya unawapa hofu waandaaji hao kwamba huenda soko la biashara yao likayumba

Mto wa kuchegama watumika kuondoa uhai wa watoto wadogo ndugu wawili. 
Mtanzania aishiye Melbourne,Australia,Charles Mihayo mwenye umri wa miaka 36,aliyekuwa akituhumiwa kwa mauaji ya binti zake wawili,amehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Mihayo ametiwa hatiani baada ya mahakama kujiridhisha kwa ushahidi uliothibitisha kwamba aliwaua binti zake ,,Indiana aliyekuwa na umri wa miaka mitatu na Savannah aliyekuwa na umri wa miaka minne kwa kuwaua kwa kuwabana kwa mito ya kulalia na hivyo kukosa hewa.
Waendesha mashtaka walisema kwamba, Mihayo alitenda kosa hilo baada ya kuingia kwenye mgogoro mzito na mama wa watoto aliyewahi kuwa mkewe kwa minajili ya kujilipiza kisasi.
Akitoa hukumu hiyo jaji wa mahakama kuu ya Victorian,Lex Lasry alisema ugomvi na mkewe haikuwa sababu ya kujiaminisha kutenda kosa la mauaji na kushangazwa na namna mtuhumiwa alivyotumia nafasi ya ugomvi na mkewe wa zamani kuwaua watoto ili kupunguza machungu yake.
Inaelezwa kuwa Mihayo alituma ujumbe mfupi wa maneno kwa mtalaka wake kumfahamisha kuwa ameshinda na anakubali kupoteza haki yake ya kuwaona watoto hao, kisha akawapiga picha watoto hao wakicheza muziki muda mfupi kabla na kuwaweka pamoja na kuwabana pumzi kwa kutumia mito ya kulalia,kisha kupiga simu polisi na walipowasili eneo la tukio, aliwaambia "nimekamilisha,nimewaua watoto wInaelezwa kuwa Mihayo alituma ujumbe mfupi wa maneno kwa mtalaka wake kumfahamisha kuwa ameshinda na anakubali kupoteza haki yake ya kuwaona watoto hao, kisha akawapiga picha watoto hao wakicheza muziki muda mfupi kabla na kuwaweka pamoja na kuwabana pumzi kwa kutumia mito ya kulalia,kisha kupiga simu polisi na walipowasili eneo la tukio, aliwaambia "nimekamilisha,nimewaua watoto wangu"
                                                  V.S

Rais Jakaya Kikwete 
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete leo atalihutubia taifa la nchi hiyo ambapo anatarajiwa kuyatolea ufafanuzi masuala nyeti yanayoligusa taifa hilo.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa na kijamii wanatabiri huenda hatua atakazozichukua dhidi mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika na ufisadi wa mamilioni ya fedha katika akaunti ya Escrow itakuwa ni moja kati ya agenda muhimu atakayoitolea ufafanuzi.
Hotuba hiyo inakuja wakati kukiwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya raia na wapinzani wakitaka hatua zaidi zichukuliwe kutekeleza azimio la bunge ambalo linatataka mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika na sakata hilo la ufisadi wawajibishwe ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.
Watu wakubwa serikalini akiwemo waziri mkuu Mizengo Pinda walihusishwa na Kashfa ya Ecrow na kutakiwa kujiuzulu 
 
Sakata la Akaunti ya Escrow liliibuliwa bungeni na mmoja wa wabunge wa bunge la Tanzania, David Kafulila na kusababisha mjadala mkali na kuamua Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kupewa jukumu la kuchunguza kashfa hiyo.
Baada ya uchunguzi kuwasilishwa katika mkutano wa bunge uliomalizika mwishoni mwa mwezi Novemba, kamati hiyo ilikuja na maazimio manane kuhusu taarifa ya ukaguzi maalum kuhusiana na miamala iliyofanyika katika akaunti ya Escrow ya Tegeta pamoja na umiliki wa kampuni ya IPTL.
Miongoni mwa maazimio ya bunge yaliwataja baadhi ya wanasiasa, mwanasheria mkuu, maafisa waandamizi wa serikali, majaji, wakuu wa taasisi za umma, viongozi wa dini, mawakili wa kujitegemea na watu binafsi kuhusika katika kashfa hii na hivyo kuagiza mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua za kisheria wahusika na wengine kuondolewa katika nyadhifa zao za kuteuliwa,tayari Mwanasheria mkuu wa serikali amekwisha jiuzulu na rais kukubali uamuzi huo.
Akaunti ya Escrow ilianzishwa katika Benki Kuu ya Tanzania ili kuhifadhi fedha, baada ya kuibuka kwa mvutano kati ya Shirika la Umeme la Tanzania, Tanesco na kampuni ya kufua umeme ya IPTL kuhusu ongezeko la mtaji wa uwekezaji, huku TANESCO ikilalamika kuwa gharama za kununua umeme kutoka kampuni ya IPTL zilikuwa za juu mno. Fedha hizo zingeendelea kutunzwa katika Akaunti hayo hadi wakati ambapo suluhisho la mvutano wa wabia hao wawili lingepatikana.
                                                    V.S
mkuu wa wilaya ya songea akifungua mkutano kati ya wataalam wa misitu na wafanyabiashara wa mazao ya misitu wilaya ya songea mkaoni Ruvuma.
Mkuu wa wilaya ya songea akitoa msisitizo wa kusimamia sheria za uvunaji wa misitu ili kuepuka kutokea kwa jangwa katika maeneo ya wilaya ya songea.


meneja wa wakala wa huduma za misitu wilaya ya songea bi Manyisye Kibona Mpokigwa  pamoja na kaimu mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya songea bwana godifrei chipakapaka.
Baadhi ya mabwana miti wilaya ya songea wakifuatlia kwa umakini mkubwa katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa maliasili wa mkoa wa Ruvuma.

wafanyabiashara wachache wakisiliza mada ya mabadiliko ya taratibu za uvunaji na biashara ya mazao ya misitu.

MAELEZO NA MATHIAS PONDAMALI.
imeelzwa kuwa utaratibu wa uvunaji wa miti kwa ajili ya mkaa,mbao na kuni ni pamoja na uvunaji huo ufanyike katika eneeo lililoruhusiwa tu,uvunaji kwa ajili ya mbao hauruhusiwi kuanusha mti kabla ya kupima kipenyo,haiuhusiwi kuchana magogo kwa kutumia msumeno wa mnyororo(chainsaw.

Lakini pia utaratibu wa usafirishaji wa mazao ya misitu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine
>kabla ya kuanza kusafirisha mazao ya misitu hakikisha umelipa ushuru wa serikali kuu na wa halmashauri ya wilaya.
>kila mfanyabiashara wa mazao ya misitu lazimaawe bna hati ya kusafirisha anapotoka sehemu moja kwenda nyingine
>Hairuhusiwi kusafirishaji mazao ya misitu yakiwemo mazao ya mkaa na kuni zaidi ya saa kumi na mbuili jioni na kabla ya saa kumi na mbili asubuhi.
>Mazao yote ya misitu kama vile mbao,mkaa,samani au kuni yatakayoyatakayosafirishwa kwa njia ya yoyote kama vile magari madogo pikipiki baiskeli,mikokoteni,baiskeli na nk.
>nyaraka zinazohusika zikaguliwe.

Thursday, 18 December 2014

















                                                                                                               V.S