
Vumbi la kinyang’anyiro cha uteuzi wa kuwania urais ndani ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM), linaanza rasmi Dodoma leo kwa wanachama wake watano
kuchukua fomu wakiomba uteuzi huo.
CCM imepanga kuanzia leo Juni 3 hadi Julai 2, mwaka huu, kuwa siku za
kuchukua na kurudisha fomu za wanachama wake wanaoomba uteuzi kuwania
urais.
Uteuzi huo ni kwa Urais wa Jamhuri ya Muungano...