Sunday, 31 August 2014

Mkazi wa Kihesa katika Manispaa ya Iringa, Peter Kalawa akiuliza swali katika mkutano wa hadhara wa Kampeni ya Kituo cha Sheria na haki za Binadamu...
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Hussein Ngaga. OFISA ushirika wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Raphael Luvanda ameonja joto ya jiwe baada ya Wanachama wa chama cha kuweka na kukopa, Mbinga Lutheran SACCOS kumjia juu na kumweleza kwamba hawana imani naye katika utendaji wa kazi zake hivyo hawamtaki kumuona akifanya kazi za ukaguzi katika...
Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG), Mhe. Anna Abdallah akifungua Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma. Katibu wa Umoja wa Wanawake Wabunge Tanzania (TWPG), Mhe....
 Wadau wa TMT wakiwa kwenye Red Carpet ndani ya Ukumbi wa Mlimani City katika FAinali ya Shindano la Kusaka Vipaji vya Uigizaji lijulikanalo Kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo  Mshindi wa Shilingi Milioni 50 za Kitanzania Alipatikana  Ceaser Daniel akiwa na Jaji wa Tanzania Movie Talents (TMT) Single Mtambalike  Kikundi Cha TMT...
Msanii wa muziki Florah Mbasha, Baada ya kufunguka mengi kuhusiana na matatizo katika ndoa yake wiki hii, ameweka wazi kuwa shughuli zake za muziki bado zinaendelea huku akiwa na albam mpya kabisa kwaajili ya wapenzi wa sanaa yake.Frorah Mbasha amesema kuwa, anamshukuru Mungu kwa kufanikisha kutoa albam mpya inayokwenda kwa jina Nipe Nguvu ya Kushinda, kazi ambayo tayari jamii imeipokea...
BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA), limetangaza mfumo mpya wa upangaji wa madaraja ya ufaulu kwa kutumia wastani wa pointi (GPA) ambao utaanza kutumika katika mtihani wa kidato cha nne 2014 na cha sita 2015.Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde, alisema kuwa mfumo huo umekuwa ukitumika katika kupanga madaraja...
Jengo lililolipuliwa. Mlipuko umeharibu jengo moja la ghorofa 4 kazkazini mashariki mwa Paris na kumuua mvulana mmoja huku watu kadhaa wakiwa hawajulikani walipo.Watano kati ya wale waliotoweka wanadaiwa kuwa watoto.Afisa mmoja wa huduma ya zima moto katika mji huo mkuu amesema haijulikani ni nini kilichosababisha mlipuko huo. Msemaji huyo amesema kuwa maafisa wa matibabu wamepelekwa...
...